Apple waleta iPhone 6 & 6 Plus , Saa na Mfumo wa Malipo

2
Sambaza

teknokona_iphone6plusLeo kampuni mashuhuri kwa utofauti na mfumo wa kipekee wa kuingiza sokoni matoleo ya simu na tableti zake siku ya leo wametambulisha simu mpya ya iPhone 6 inayokuja na matoleo mawili ya kitofauti – iPhone 6 na iPhone 6 Plus. Pia Apple wametambulisha saa janja itakayokuwa inafahamika kama Apple Watch, kitu cha tatu ni mfumo mpya wa malipo ambao mtumiaji wa iPhone ataweza kulipia huduma au bidhaa kutumia simu yake yenye akaunti ya Apple ID iliyounganishwa na akaunti ya benki (Visa, MasterCard). Fahamu haya yote hapa.

iPhone 6 na iPhone 6 Plus

Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni pamoja na kukuza ukubwa wa simu za iPhone. iPhone 5 ilikuwa na kioo cha ukubwa wa inchi 4 (iPhone 4 ilikuwa na kioo cha inchi 3.5), iPhone 6 inakuja na kioo cha ukubwa wa inchi 4.7 na iPhone 6 Plus kioo cha ukubwa wa inchi 5.5. Haya ni mabadiliko makubwa kwani Apple huko zamani walikuwa wakiongea dhidi ya simu zenye vioo vikubwa lakini hivi karibuni wameshuhudia simu za Android zenye vioo vikubwa zikifanya vizuri sokoni mfano wa Samsung Galaxy na zinginezo. Tazama kwa ufupi sifa za simu hizi;

Wembamba wa iPhone 6 na 6 Plus ukilinganisha na iPhone 5S

forex valutakurs usd Wembamba wa iPhone 6 na 6 Plus ukilinganisha na iPhone 5S

Sifa za iPhone 6
SOMA PIA:  Apple yapunguza bei ya betri ya simu zake
Sifa za iPhone 6Plus
teknokona_iphone6

see Mlinganisho wa Vioo vya iPhone 6 na iPhone 6 Plus na iPhone 5S

Sifa za Ujumla

follow 64-bit A8 chip: Apple wamejitaidi katika kuzifanya iPhone 6 kuwa kati ya simu za mwanzo zenye uwezo mkubwa kiufanisi kwa kutumia teknolojia ya 64bit na chip zenye nguvu A8. Pamoja na hii zimewekwa pia http://madanha.ir/aribos/arini/3093 M8 ‘co-processor’ zenye kusaidiana na chip za A8 katika kuhakikisha simu zinakuwa katika ufanisi wa hali ya juu bila kutumia chaji nyingi na hivyo kuongeza muda wa betri kukaa na chaji.

SOMA PIA:  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

Kamera ya 8 – Megapixel: Kamera nayo imeboreshwa kwa kuongezwa uwezo wa kuboresha muonekano bila ya mtumiaji kuhusika (sensors), hii ikiwa ni pamoja kuboresha picha kutokana na hali ya mwanga au rangi pale picha inapopigwa.

Intaneti ya kasi zaidi? -LTE! – Tatizo ni tulipo, ila simu za iPhone 6 kupitia teknolojia ya LTE zinaruhusu hadi intaneti ya kasi ya MB 150 kwa sekunde ikilinganishwa na iPhone 5 na zinginezo zilizo na uwezo wa MB 100 kwa sekunde.

Betri yenye uwezo zaidi: Apple wamedai ya kwamba batri za iPhone 6 na 6PLus zinakuwa na uwezo mkubwa zaidi kulinganisha na za iPhone 5. Hapa hatutaki kwenda kwa undani sana…

Mlinganisho wa Uwezo wa Kudumu na Chaji

Mlinganisho wa Uwezo wa Kudumu na Chaji

Teknolojia ya QuickType kwenye ‘keyboard’ na uwezo wa kutumia ‘keyboard’ mpya.  Kupitia iOS 8 keyboard itakuwa inarekodi na kutabiri maneno kwa jinsi unavyoitumia, na pia Apple wataruhusu watengenezaji wengine wa Apps kuweza kubuni na kutengeneza Apps za keyboard zinazoweza kutumia kama mbadala wa keyboard za iOS 8.

SOMA PIA:  Ijue Simu mpya ya mkunjo yenye vioo viwili ya Samsung Galaxy W2018

MFUMO WA MALIPO

Kwa kutumia teknolojia inayofahamika kama NFC  (Near-field communications) watumiaji wa iPhone 6 wataweza kufanya malipo mbalimbali ya bidhaa au huduma kwenye sehemu zinazotumia kifaa chenye kuweza kuwasiliana na simu zenye NFC. Hii ni juhudi ya Apple kuingia katika ushindani mkali na makampuni kama Amazoni na Paypal.

APPLE WATCH

saa_apple_watchKumiliki saa janja hii itakugharimu takribani Tsh Laki 6 ($350)…upo hapo? Na kuweza kuitumia inakuitaji uwe unamiliki iPhone 5 au 6, kwani ni kupitia simu hizi ndio utaweza kufanya nayo mawasiliano. Pia kupitia ushirikiano na kampuni zingine Apple imewezesha saa hizi kukuonesha vitu kama ‘status’ za Facebook , matokeo ya michezo au kukuonesha wapi umepaki gari lenye mfumo wa iOS kama BMW.

Je unadhani toleo la iPhone 6 ni kubwa sana? Apple wameleta kitu chochote kipya na cha kuvutia kwako kupitia simu hizi?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

2 Comments

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com