Pale kampuni inapouza lazima ifarijike na swala hilo na pale inapouza sana kuliko mategemeo yake inaweza ikawa ni sherehe moja kwa moja.
Hiki ndiko kilichotekea katika kampuni ya Apple, Apple watch imevunja rekodi ya mauzo ukilinganisha na hapo nyuma.
Labda kwa kuwa hiki ni kipindi cha likizo ndio maana mauzo hayo yamepanda kwa kiasi kikubwa mpaka kampuni hiyo kushtuka. kwa kawaida bidhaa za iPad na iWatch huwa zinapata muamko wa mauzo mdogo kulinganisha na bidhaa zake zile za iPhone na kompyuta zake.
“Taarifa zetu zinaonyesha kuwa Apple Watch inafanya vizuri na inaonekana kuwa ni moja kati ya zawadi kuu za sikuku ya mwaka huu” – Tim Cook.
Tim cook aliongezea kuwa saa hiyo ilipanda mauzo na kuvunja rekodi kwani mauzo hayo yalikuwa makubwa sana katika wiki ya sikuu ukilinganisha na mauzo katika wiki nyingine yeyote katika historia ya kuuza saa hizo.
Japokuwa muongozi huyo wa kampuni Tim Cook hajaweka wazi kuwa mauzo hayo yamepanda kwa asilimia ngapi mpaka kufika wapi lakini cha kujua ni kwamba yamepanda tuu.
Hili ni jambo zuri kabisa kwa kampuni hiyo ya Apple, kumbuka hapo mwanzo tumeshuhudia kampuni hii kutofanya vizuri katika baadhi ya bidhaa na kuwa na mauzo ya kawaida sana kulinganisha na bidhaa zake zingine.
Tuandikie hapo chini sehemu ya comment, wew umelipokea vipi jambo hili. ningependa kusikia kutoka kwako.