Apple yafanya masasisho kwenye iOS 11.1 kurekebisha mambo mbalimbali - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple yafanya masasisho kwenye iOS 11.1 kurekebisha mambo mbalimbali

1
Sambaza

Utakumbuka mapema wiki hii tuliandika makala kuhusu toleo la iOS 11.1 kuwa na tatizo ambalo lilitokea kukera watu wengi hasa wale ambao wanatumia toleo la iOS 11.1 kwenye vifaa vyao vilivyotengenezwa na Apple.

source

Hii inakuwa ni habari njema sana kwa watumiaji wa vifaa vya Apple Apple kwani walipata shida walipokuwa wanataka kuandika http://hsifinancial.com/economic_evolution.html/https://linkedin.com/in/wesforster neno linaloanzia na herufi “i” na badala ya herufi “i” kutokea inatokea herufi “A” ikifuatiwa na alama ya kiulizo!. Jambo hilo lilileta changamoto kwa wengi ingawa Apple wlitoa mbinu ya kuweza kuliondoa tatizo lakini haikuwa ni sulihisho la kudumu.

Katika masasisho ambayo Apple imetoa imehakikisha kabisa inatatua kabisa lile tatizo la herufi “i” kutokea vinginevyo (bila kutokea herufi/alama isiyostahili).

Tatizo la herufi “i” kubadilika na kuwa herufi “A” pamoja na alama ya kiulizo iliyo ndani ya kiboksi.

Toleo la iOS 11.1.1 limekuja na nini kingine cha ziada?

Ndio, kwanza ni vyema ukafahamu kuwa masasisho katika toleo la iOS 11.1 ni muendelezo tu na toleo rasmi kwa watumiaji wa vifaa vya Apple mathalani simu za iPhone (kuanzia iPhone 5s na kuendelea) limeboreshwa na kuwa where can you buy generic Finax “iOS 11.1.1” ambalo mbali na kuondoa tatizo la kwenye herufi “i” pia limeweka mambo sawa kwenye “Hey, Siri” (Kisaidizi binafsi kwenye bidhaa za Apple) ambayo nayo ilikuwa na kasoro ndogondogo kwa baadhi ya vifaa.

Masasisho ya iOS 11.1.1 pia yamekuja na emoji mpya 70 na kuruhusu 3D Touch Apple Switcher ambapo kama kawaida si kila kifaa cha Apple kinaweza kupata masasisho hayo. Kwa upande wa simu janja ni kuanzia iPhone 5s na kwa upande wa iPad ni iPad Air na matoleo yaliyofuataiPad Mini 2 na matoleo yalioendelea pamoja na kizazi cha sita cha iPod za mguso.

Kufanya kifaa unachotumia kuweza kupata masasisho hayo (kama ni kifaa cha Apple) kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha una kifurushi cha intaneti kinachoridhisha (kuanzia MB 100 na kuendelea) pamoja na intaneti ambayo mtandao wake haushuki jambo linaloweza kusababisha kuharibu simu yako hata kama utatumia WiFi kupata masasisho hayo.

Kufanya masasisho kwenye kifaa cha Apple unaingia Settings > General > Software Update kisha unafuata maelekezo utakayoyaona baada ya hapo.

Kikubwa cha kuzingatia kabla ya kufanya masasisho kwenye bidhaa ya Apple unahakikisha kifaa husika kina chaji kuanzia 50% au zaidi, fanya backup ya vitu vilivyopo kwenye kifaa hicho. Je, wewe ni tayari unatumia toleo la iOS 11.1.1 kwenye kifaa chako?

Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|