Apple yaongoza mauzo kwa soko la Marekani robo ya tatu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple yaongoza mauzo kwa soko la Marekani robo ya tatu

0
Sambaza

Kulingana na ripoti ya Strategy Analytics kampuni ya Apple imeendelea kuongoza mauzo ya simu zake janja kwa soko la nchi ya Marekani katika robo tatu ya mwaka 2017.

watch Hata hivyo mauzo ya simu hizo yameshuka kulingana na ya mwaka jana ambapo mwaka huu waliuza simu milioni 12 na mwaka jana milioni 13 kwa robo ya tatu ya mwaka.  buy lasix from canada iPhone 8 na iPhone 8 Plus zimeonekana kupata changamoto za mauzo kwa kuwa watu wengi walikuwa wanasubiri go to link iPhone X ambazo zimeanza kuuzwa Novemba 3 katika soko la Marekani.

Apple yaongoza mauzo kwa soko la Marekani robo ya tatu

Apple yaongoza mauzo kwa soko la Marekani robo ya tatu: Watabiri wanasema pengine robo ya nne wanaweza kuongeza mauzo zaidi kwa sababu ya iPhone X iliyokuwa ikisubiriwa na wengi na vilevile sikukuu za mwisho wa mwaka zitachangia kuuzwa pia.

Samsung iliendelea kuwa nafasi ya pili kwa kusafirisha simu milioni 9.9 sawa na asilimia 25 ya soko lote la marekani na mauzo hayo yamepanda kulingana na mwaka jana walipouza simu milioni 9.7 katika robo tatu ya mwaka.

Licha ya kuwa nafasi ya pili kwa soko la Marekani lakini Samsung ndio inaongoza kwa mauzo duniani kote. Simu za LG, ZTE na Motorola zilikuwa kati ya nafasi tano za juu katika soko la mauzo. Mauzo ya Motorola yaliongezeka mara mbili kutoka milioni 1.1 mpaka milioni 2.1 na hivyo kuwa na asilimia 5 ya mauzo kwa soko la Marekani.

INAYOHUSIANA  Kingo Root: Programu/App ya Kuroot Simu za Android na Windows

Motorola wameonekana kufanya vizuri zaidi katika soko la Marekani kwa robo ya tatu ya mwaka 2017 kulingana wa simu zingine. Je, ni kampuni gani hapo juu haijawahi ‘kukuangusha’ kila inapotoa bidhaa mpya?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.