Kampuni ya Apple imefanya vizuri katika soko kwa kuuza saa janja (Apple Watch) zake katika robo tatu ya mwaka 2017 kulingana taarifa ya Canalys iliyotoka karibuni.
Apple imeweza kuuza saa janja takribani milioni 3.9 kwa familia ya saa zake za Apple watch series 3 ambapo ni sawa na asilimia 23 ya saa zote zilizouzwa katika robo ya tatu. Jumla ya saa janja zipatazo milioni 17.3 ziliuzwa ambapo Apple imewazidi wapinzani wake wa karibu kutoka Xiaomi na Fitbit kwa pengo dogo. Mauzo ya saa za Apple yameshuka kulingana na ya mwaka jana.
Xiaomi imeweza kuuza saa janja zake zipatazo milioni 3.6 sawa na asilimia 21 katika robo tatu ya 2017 wakati Fitbit walifanikiwa kuuza saa janja milioni 3.5 sawa na asilimia 20. Watafiti wanaamini mauzo ya saa janja za Apple katika robo ya mwisho ya 2017 yanaweza kushuka kutokana na ushindani mkubwa unaopata kutoka kwa Xiaomi na Fitbit. Hata hivyo wachambuzi hao wamesema Apple wana uwiano mzuri wa mauzo ya simu na saa zake.
Mauzo ya saa janja kati ya makampuni vinara.
>Apple- Huuza saa janja moja kila baada ya simu janja 7 kuuzwa
>Samsung- Huuza saa janja moja kila baada ya simu janja 23 kuuzwa
>Huawei- Huuza saa janja moja kila baada ya simu janja 14 kuuzwa