Betri za simu za Apple daima zimekuwa si bei rahisi lakini mwaka unaisha huku wakilazimika kupunguza bei ya betri za simu janja kutokana na makosa yao wenyewe kwenda kwa wateja wake.
Siku kadhaa zilizopita Apple iliachia sasisho fulani kwenda kwenye simu zake (iPhone) jambo lilipelekea utendaji wa kazi kwa iPhone 6, 6S, 7 na SE kwa betri ambazo ni za muda mrefu kufanya simu hizo kuwa nzito na kutumia kiwango kikubwa cha chaji kutokana na sasisho hilo.
Apple imepunguza bei ya betri za simu zake kwa $50 kutoka $79 (Tsh. 177,750) mpaka $29 (Tsh. 65,250) kutokana na kuruhusu sasisho ambalo limesababisha karaha bila kujali madhara/faida ya maboresho waliyoyatoa.
Baada ya sasisho hilo kuruhusiwa lilipelekea simu za iPhone ambzo betri zake ni za muda mrefu kupelekea simu kuzima bila kutarajia kutokana na betri hizo za Lithium kutopokea uwiano mzuri wa kiwango cha nguvu kwa betri husika.
Apple imekiri na kuomba msamaha kutokana na kusababbisha baadhi ya simu za wateja wake kutofanya kazi vizuri mpaka pale walipobadilisha betri kwenye simu zao. Kwa mujibu wa tamko walitoa wanasema hawakuwa na nia mbaya kwa wateja wa simu zilizoathiriwa kutokana na sasisho hilo.