Kampuni ya Apple yapunguza ushuru kwa wateja wanawauzia, kununua app katika simu janja au bidhaa nyingine yoyote kutoka App store.
Apple imekuwa ikitoza ushuru wa juu kwenye apps zake kwa zaidi ya miaka saba lakini kwa mara ya kwanza Apple wamepunguza ushuru wa kile kinachopatikana cha ziada kwa sharti moja tu kwamba mtu aliyenunua app hiyo atumie kwa zaidi ya mwaka mmoja; mapato yatakayotokana na mauzo ya apps hiyo yatagawanywa kwa asilimia 85/15.
Iwapo hata nusu ya subscribers bado wanaendelea kulipia apps wanazozitumia ambao kwa makadirio mapato yake yatafikia $15m, Spotify itaweza kupata $15m kama mgao kutokana na ushuru wa malipo yatokanayo na mauzo ya programu tumishi wanazozimiliki.