´╗┐ Apple yashauriwa kutoacha kuweka sehemu ya 'EarPhone Jack' kwenye iPhone 7

Apple yashauriwa kutoacha kuweka sehemu ya ‘EarPhone Jack’ kwenye iPhone 7

2
Sambaza

Apple wana mpango wa kutoweka sehemu ya kuchomeka kwenye iPhone 7 inayotarajiwa kutoka hivi karibuni; wameshauriwa kuweka sehemu hiyo ya kuchomeka EarPhone kwenye simu janja hiyo.

Steve wozniak

priligy generic cheap Steve Wozniak-Mmoja ya waanzilishi wa kampuni ijulikanayo kama Apple.

Ushauriwa huo ulitolewa na mmoja wa waanzilishi wa Apple Bw.┬áSteve Wozniak na kusema kuwa kuondoa sehemu ya kuchomeka earphone inayofahamika kama ‘jack’ itakuwa ni kosa kubwa kitu ambacho kinaweza kuigharimu kampuni.

http://cherokeestripridingclub.org/photo-gallery/ Apple wanataka kuondoa mfumo huo na kisha kutambulisha mchomekeo wa earphone wa kisasa zaidi utakaokuwa unatumia eneo lile lile linalotumiwa kwa ajili ya kuchajia simu na kuchomekea USB kuunganisha na kompyuta.

Ni kwanini si vyema kuondoa sehemu ya kuchomeka EarPhone (Earphone jack)?

  • Imekuwa ni tamaduni ya Apple kuweka sehemu ya kuchoka eaphone tangu kuanzishwa kwa simu janja hizo mwaka 2007.
  • Uwepo wa ‘Earphone Jack’ kumerahisisha watu wengi kuweza kusikiliza muziki na kama sehemu hiyo haitakuwepo kwenye iPhone 7 basi simu hiyo inaweza isiwavutie wengi.
  • Kama EarPhone Jack ikiondolewa basi watumiaji wa iPhone 7 watabidi wanunue earphones zisizotumia waya (inasemekana Apple wanatengeneza wireless earphones) kitu ambacho zinaweza kuwa ghali kama ilivyo kawaida ya bidhaa za Apple.
  • Haitokuwa na muonekano wa kuvutia iwapo sehemu hiyo ya kuchomeka earphone ikiondolewa na sababu hiyo inaweza kushusha mauzo ya simu hiyo.
iPhone 7

can i order flagyl online iPhone 7 bila ya sehemu ya kuchomeka earphone(Earphone jack).

 

INAYOHUSIANA  Namba za madereva wa Uber kutoonekana Kenya

Watu wengi wanasubiri muendelezo wa simu jaja hiyo katika familia ya iPhone ila ni muhimu kuwa tayari kutumia iPhone 7 bila sehemu ya kuchomeka earphone ya teknolojia iliyozoeleka, iwapo wakipuuza ushauri waliopewa na Steve Wozniak. Simu hiyo inatarajiwa kutoka wiki ya pili ya mwezi Sept.

Nini maoni yako kuhusu iPhone 7 kutokuwa na sehemu ya kuchomekea EarPhone? Je, unadhani itawavutia wengi kama simu za awali? TeknoKona siku zote inakuletea makala za kuvutia.

Vyanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|