Apple, kampuni nguli katika maswala ya teknolojia kwa ujumla imetoa taarifa ya gemu na App bora kwa mwaka 2017, Haikuishia hapo bado imeenda mbele zaidi na kutoa App,gemu na miziki maarufu zaidi.
Watumiaji wa iPhone na iPad hii list inawahusu moja kwa moja kwani wamekua wakipakua vitu hivi katika soko maarufu la App store.
App Na Gemu – iPhone
App Ya Mwaka ni Calm, App hii ni maarufu sana na uwezo wake ni kusaidia watu katika tiba. Calm ipo katika kipengele cha Afya na ni moja kati ya zile App ambazo zinamsaidia mtu kuwa na mwili ambao upo fiti. Calm inapatikana bure kabisa ila ndani ya App yenyewe kuna vitu unaweza kununua ili kuendelea kuifurahia zaidi.
Gemu Ya Mwaka ni Splitter Critters ambapo gemu hii ni ya kunoa akili ambayo iko katika mfumo wa 2D. Gemu hii inauzwa dola 2.99 za kimarekani.
App Na gemu – iPad
App ya Mwaka ni Affinity Photo,ambayo ni maarufu sana kwa kuhariri (edit) picha. App hii inasapoti mpaka mafaili yenye ubora wa RAW. Vile vile App hii ina gharama kubwa maana ilikua inauzwa dola 19.99 lakini baada ya kutajwa kama App ya mwaka watengenezaji wake wameamua kuishusha mpaka dola 9.99 za kimarekani.
Gemu Ya Mwaka ni The Witness, ambapo hii nayo pia ni Gemu ya kunoa akili. Ndani ya gemu hii utakutana na vikwazo vingi ambavyo vitakulazimu kunoa bongo. Gemu hii inapatikana kwa dola za kimarekani 9.99.
Maarufu Kwa Apple (2017) Kwa Ujumla
Apps
- Bitmoji
- Snapchat,
- YouTube
- Messenger
Gemu
- Super Mario Run
- 8 Ball Pool
- Snake VS Block
- Ballz
- Word Cookies.
Apple Music
Albamu Maarufu –More Life ya Drake
Muziki Maarufu – Shape of You ya Ed Sheeran
ITunes (Sinema)
- Moana
- Rogue One: A Star Wars Story
- Wonder Woman
iTunes (Michezo Ya Kuigiza) – TV Series
- Game of Thrones
- The Walking Dead
Hizo ndizo list ambazo zimetolewa na Apple katika kuonyesha nani kashika kileleni kwa mwaka 2017. Ni kawaida kwa Apple kutoa list hizi kila inapofika mwisho wa mwaka. Je ni App gani au gemu unahisi ilibidi iwe katika list hii?