Apple yatetea uamuzi wake kuondoa App za VPN China

1

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Apple, Tim Cook ametetea uamuzi wa kampuni yake kuondoa App za VPN kutoka App Store ya China.

Apple yatetea uamuzi wake kupitia kiongozi wake Tim Cook ambaye amesema wanalazimika kufuata mahitaji ya Serikali ya China kama wanavyofanya katika nchi zingine. “Kama tunavyofanya katika nchi zingine, tunafuata sheria popote tunapofanya biashara”, alisema.

App za VPN zinasaidia kuwaruhusu watumiaji wa Mitandao kuweza kuzifikia Tovuti zilizozuiliwa katika maeneo yao.

Apps za VPN kwa simu za iPhone nchini China

Apps za VPN kwa simu za iPhone nchini China ni marufuku

Wafanyabiashara na raia wa China wanaweza kuvuka vikwazo vya serikali yao kwa kupata na kuweza kuingia mitandao iliyozuiwa na serikali kwa kutumia App za VPN.

  • Nchi ya China inayoongozwa na chama cha kikomunisti imekuwa ikiimarisha udhibiti wa mitandao na vyombo vya habari vya mitandaoni na michezo ya kubahatisha.
  • Ili kuweza kuendesha huduma za VPN nchini China ni lazima watengezaji wa App wapate kibali cha serikali.
  • Mnamo mwaka wa 2016, Umoja wa Mataifa ulipitisha tamko lisilo la kisheria kuwa upatikanaji wa intaneti ni haki ya binadamu ambayo lazima ipatikane bila ya kuzuizi chochote.

Kifungu hicho kinasema kwamba Umoja wa Mataifa unapinga hatua za “kuzuia kwa makusudi au kuharibu upatikanaji au usambazaji wa habari mitandaoni” na kwamba kufanya hivyo ni “kukiuka sheria ya kimataifa ya haki za binadamu”

Nchi ya China pamoja na Urusi, Afrika Kusini na Saudi Arabia zinapingana na azimio hilo la Umoja wa Mataifa.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com