Apple yatoa MacBook Pro (2017) iliyo bora zaidi

1
Sambaza

Katika moja ya bidhaa ghali sana kwa vifaa vya Apple kompyuta ni moja ya bidhaa hizo ambazo hazijawahi kuwa bei rahisi tangu huko nyuma hata mpaka sasa.

Baada ya toleo la mwaka 2016 kwa kompyuta mpakato za MacBook Pro kukosolewa sana hasa kwenye upande wa betri Apple imejibu. Toleo la MacBook Pro (2017) limekuja na kile ambacho kililalamikiwa na wateja walinunua toleo la MacBook Pro la mwaka 2016 lakini kama kawaida si rahisi.

Hakuna mabadiliko makubwa kati ya MacBook Pro (2017) na ile ya mwaka 2016 isipokuwa tu toleo la mwaka 2017 linakuja na kizazi cha saba cha prosesa (chips) za Intel, toleo jipya la MacOS High Sierra na uwezo wa betri kukaa na chaji kwa muda mrefu.

Muonekano wa MacBook Pro ikiwa imefunuliwa.

Undani wa mambo yaliyoboreshwa kwenye MacBook Pro (2017).

see >Kizazi cha saba cha chips za Intel. Kwa uamuzi wa kutumia chips za Intel ambazo ni za kizazi cha 7 ni jambo zuri sana likimaanisha MacBook Pro (2017) itakuwa yenye kasi na uwezo wa hali ya juu tofauti na toleo la mwaka 2016 ambalo lilikuwa na chips za Intel kutoka kizazi cha sita.

SOMA PIA:  Simu ndogo unayoweza 'Kuizungushazungusha'

>Toleo jipya la MacOS High SierraToleo hili jipya la programu endeshaji katika utumaji wa mafaili hapa inatuma kwa kasi sana. MacBook Pro (2017) inasifika kwa kukuwezesha kufanya shughuli za uhariri wa picha, video (hata zile za 4K) bila wasiwasi wa kuhofia umeme wa kwenye kompyuta kuisha kabla ya wewe hujamaliza kazi ya uhariri wa picha/video.

Kitu kizuri hakikosi kasoro ingawa ni moja ya kompyuta bora kwa mwaka 2017 lakini toleo hili jipya la MacBook Pro haina teknolojia ya USB Type-A.

>Uwezo wa betri. Katika kulinganisha toleo la mwaka 2016 na lile la mwaka 2017 imebainika toleo la mwaka 2017 la MacBook Pro limeongezewa saa mbili za ziada kwa upande wa betri kulinganisha na toleo la mwaka 2016 la MacBook Pro.

SOMA PIA:  Undani wa namba '108' kwenye app ya Siri #Maujanja

Kwa ujumla toleo la MacBook Pro (2017) linadumu na chaji kwa karibu saa 8 ukiwa imechajiwa na betri likajaa kabisa. Matumizi yake yanaweza kujumisha mwanga wa kwenye kioo wa mpaka 70%, ukiwa umefungua kurasa 5-10 kwenye kivinjari pamoja na vitu vingine kama Typora for text, Wire for chat, Mac Mail for email, Reeder for RSS feeds na Pixelmator.

Sifa nyinginezo kwa ufupi.

  • Kioo: 13.3in LCD 2560×1600 (227 ppi)
  • Prosesa: Intel Core i5 or i7 (kizazi cha saba)
  • RAM: 8 au 16GB
  • Diski uhifadhi: 128, 256, 512GB au 1TB
  • Programu endeshaji: macOS High Sierra
  • Kamera: 720p FaceTime HD camera
  • Uwezo wa kwenye intaneti: Intel Iris 650, Wi-Fiac, Bluetooth 4.2, USB-C, Thunderbolt 3, sehemu ya kuchomekea spika za masikioni
  • Ukubwa: 212.4 x 304.1 x 14.9mm
  • Uzito: 1.37kg
SOMA PIA:  Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake #Uchambuzi

MacBook Pro zipo za aina mbili, yenye kioo cha mgusho ambayo ni $2,302|Tsh. 5,179,500 na ambayo kioo chake sio cha mguso ni $1,644|Tsh. 3,699,000. Haya toleo jipya ndio hilo na limeboreshwa vilivyo, tupe maoni yako wewe msomaji wetu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com