Apps Zilizoongoza Kushushwa App Store 2014!

0
Sambaza

Soko la Apps la Apple lina App milioni 1.3  na ina zaidi ya mapakuo (downloads) bilioni 85 tangia kuanzishwa kwa App Store mwaka 2010. Soko la App Store ni la pili kwa ukubwa kufuatiwa na lile namba moja (Google Play Store). Licha ya Hivyo, Apps nyingi zikiwa zinatoka zianzia katika soko la App Store kisha maeneo (masoko) mengine mfano Gemu la Temple run hata na Gemu la Candycrush na mengineyo.

app_store_hd_widescreen_wallpapers_1920x1200Kampuni ya Apple imetoa orodha ya Apps zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2014  na Teknokona tunayo listi ya hizo App hapa.

Na.01. Facebook Messenger;  Miezi kadhaa iliyopita Facebook iliwaambia watumiaji kuwa inabidi wadownload App nyingine (Facebook Messenger) tofauti na App ya Facebook yenyewe, Watumiaji wengi walikasirika kwa taarifa hiyo kwa sababu iliwalazimu kuwa na Apps mbili. Baada ya mda hasira ziliisha na mamilioni ya watu walikimbilia katika App store na kuidownload Facebook messenger kwa lengo la kuendeleza mazungumzo yao ya facebook.Kwa hiyo hivi inakushangaza kuwa Facebook ndio App inayoongoza kushushwa kwa mwaka katika iPhone?.

SOMA PIA:  PowerShake: Teknolojia ya kushare chaji kwa kutumia Wi-Fi #Maujanja

Na.02. SnapChat; App ya meseji za kupotea ilianzishwa mwaka 2011. Wengi walizanii haitaweza kujipatia jina kama Apps zingine kubwa duniani. Picha Milioni 700 zinatumwa kila siku na watumiaji wa Snapchat kwa siku, Mmmh hizo ni Snap nyingi sana!

Na.03. Youtube; Site namba moja duniani kwa video. inawafikia watu bilioni 1 kwa mwezi

Na.04. Facebook; Mtandao mkubwa zaidi wa kijamii ambao una watu wengi zaidi (bilioni 1.3)

Na.05. Instagram; hapa ndipo picha milioni 60 zinakua ‘shared’ kwa siku. App hii ilizidi kuwa maarufu baada ya kuchukuliwa na facebook

SOMA PIA:  Mkurugenzi wa Apple ameanza kutumia iPhone 8 ambayo haijazinduliwa rasmi?

Na.06. Free music with Pandora; Jumba la redio za kimtandao duniani

Na.07. Google Maps; Ramani ya dunia nzima katika kifaa chako chenye uwezo wa kuingia mtandaoni

Na.08. Flipagram; App ilianziswa mwishoni mwa mwaka 2013, inakuwezesha kugeuza picha zako za Facebook na Instagram kuwa katika video za stori.

Na.09. Spotify; Kwa miziki mingi ya mtandaoni. Bonyeza Play kwa ajili ya ‘live streaming’

Na.10. 2048; Gemu linalosisha namba (mahesabu) na hivyo linahitaji akili nyingi katika kulicheza. Pia wahariri wa Apple wamesema ndio gemu bora la mwaka.

SOMA PIA:  Bill Gates ajiunga mtandao wa Instagram akiwa nchini Tanzania

App Zilizo Ongoza Kushushwa Katika iPad Kwa Mwaka

1. YouTube

2. Netflix

3. Calculator for iPad

4. Skype

5. Microsoft Word

6. Facebook Messenger

7. Facebook

8. Candy Crush Saga

9. Chrome browser

10. Clash of Clans

Apple kupita soko lake la App store imekua ikiwapataia watumiaji wa simu na vifaa vyake vingine kuweza kushusha Apps za bure hata zile za kuuzwa kwa kipindi kirefu sasa.

 Ifuate TEKNOKONA na  huku Twitter, Facebook na Instagram tafadhali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com