´╗┐ Apps za Android zaanza kutumika katika Laptop za Chrome OS

Apps za Android zaanza kutumika katika Laptop za Chrome OS

0
Sambaza

Kompyuta zinazoendeshwa kwa Chrome OS ambayo inatengenezwa na Google sasa zimepewa uwezo wa kutumia apps za Android ambazo pia zinatumika na simu janja, kwa kuanzia ni kompyuta za aina tatu tu ndizo ambazo zinaweza kutumia app hizi lakini baadaye kompyuta zote zitapewa uwezo huu.

source url

Apps za android laptop za chrome

http://nexmachine.com/blog/ Muonekano wa Desktop ya Chromebook.

http://coversbykaren.com/?attachment_id=662 Kompyuta ambazo zinaendeshwa na OS ya Chrome (ambayo inatengenezwa na Google ambao ndio watengenezaji wa Android) pia zinajulikana kwa jina la Chromebooks, kompyuta hizi zinatofautiana sana na kompyuta ambazo zinaendeshwa na OS za windows ama zile zinazoendeshwa na Mac OS.

Soma zaidi: Zijue Laptop zinazoendeshwa na ‘Google Chrome OS’ Maarufu kama Chromebooks!

INAYOHUSIANA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Zilikuwepo tetesi kwamba soko la apps za Android  litanza kupatikana kwa watumiaji wa Chrome OS kwa muda mrefu na leo tetesi hizo zimethibitishwa baada ya Google kuruhusu soko hilo kupatikana katika baadhi ya kompyuta ambazo zinatumia Chrome OS.

4-3-skype-on-chrome-os-100444158-orig

Muonekano wa app ya Skype ikiwa inafanya kazi katika Chromebook.

Kwa mujibu wa tangazo kutoka Google ni kwamba kwa Apps za Android zitapatikana kwanza katika aina tatu za kompyuta kabla ya kuanza kupatiana katika aina nyingine za kompyuta , orodha na ratiba ya app hizi kufikia kompyuta mbalimbali zinapatikana HAPA.

Hii ni habari nzuri kwa kuwa apps hizo zitaongeza urahisi wa kutumia kompyuta hizi, bado hatujajaribu huduma hii lakini pindi tutakapoipata basi tutaijaribu na kuandika tathmini yetu.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.