Apps Za Mahusiano Zahusishwa na Ongezeko la Maambukizi ya Magonjwa ya Ngono

1
Sambaza

Huko nchini Uingereza apps za kutafuta mahusiano na watu wapya zimehusishwa na ongezeka kubwa la magonjwa ya ngono hii ikiwa ni pamoja na UKIMWI, Kisonono na Kaswende.

Apps kama vile Tinder na Happn zimetajwa kama apps zinazochangia usambazaji wa magonjwa ya ngono.

“Kwa kutumia apps za mahusiano mambo yanakuwa mepesi na ya haraka….hivyo unaweza kufanya ngono mara nyingi kwa siku utakavyopenda wewe…na watu tofauti..bila kufahamu wao wana magonjwa gani wanayokuficha.”

Apps za Kutafuta Marafiki wapya wa kimapenzi zinazidi kupata watumiaji wapya kila siku

Hii ni Tinder. – Apps za Kutafuta Marafiki wapya wa kimapenzi zinazidi kupata watumiaji wapya kila siku

Madai hayo yalitajwa na daktari anayeheshimika nchini Uingereza, Bwana Peter Greenhouse. Takwimu kutoka shirika la Afya la nchini humo linaonesha kuna ukuaji wa maambukizi ya magonjwa ya ngono hasa hasa Kisonono na Kaswende.

SOMA PIA:  Roboti atakayeweza kushiriki tendo la kujamiiana! #Teknolojia

Lakini umoja wa watengenezaji na watumiaji wa apps na mitandao ya mahusiano nchini humo (The Online Dating Association) wamempinga Bwana Peter Greenshouse huku wakidai hakuna uhusiano wa ongezeko la magonjwa ya ngono nchini humo na umaarufu unaokua wa huduma za mahusiano mitandaoni.

Bwana Peter Greenshouse alitetea tafiti yake huku akisema ‘unaweza kubalidilisha wapenzi/wenzi kwa haraka zaidi kwa utumiaji wa apps za mahusiano, na hili linaongeza zaidi uwezekano wa kupata magonjwa ya ngono’

SOMA PIA:  Snapchat Kuleta 'Link' Na 'Background' Katika Stories!

Umoja wa watengenezaji na watumiaji wa huduma za mahusiano kupitia apps kama Tinder na Happn wanapinga ripoti hiyo huku wakisema tatizo sio apps bali ni watu walioamua kusambaza magonjwa hayo.

Bado pia baadhi ya watumiaji wa huduma za apps hizo wanaamini ni kweli ya kwamba apps hizo zinachangia kufanya ukuaji wa kasi wa maambukizi ya magonjwa ya ngono.

Bwana Kenny Mukendi mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mtumiaji wa apps za mahusiano aliye jijini London alisema;

SOMA PIA:  Instagram kuja na app kwa ajili ya kuchati tu

“Kwa kutumia apps za mahusiano mambo yanakuwa mepesi na ya haraka….hivyo unaweza kufanya ngono mara nyingi kwa siku utakavyopenda wewe…na watu tofauti..bila kufahamu wao wana magonjwa gani wanayokuficha.”

“Yaani inakuwa ni kwa urahisi na kwa haraka, na ni jambo lisilopingika chochote kinachoweza patikana kwa urahisi kwa na kwa haraka huwa si salama” – aliongeza.

Je wewe ni mtumiaji wa apps za kutafuta watu wapya kwa ajili ya mawasiliano kama Tinder n.k? Je unafikiri ni kweli ya kwamba kuna uhusiano wowote kati ya utumiaji wa apps hizo na hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono? Tuambie.

[Makala hii imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali]

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Apps Za Mahusiano Zahusishwa na Ongezeko la Maambukizi ya Magonjwa ya Ngono | Teknolojia

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com