Apps za wanyama zawekewa katazo kulinda usalama wa wnyama pori - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apps za wanyama zawekewa katazo kulinda usalama wa wnyama pori

0
Sambaza

Programu tumishi ambazo zinaelezea kuhusu wanyama zimeonekana kuzorotesha biashara ya utalii na hivyo serikali ya Afrika Kusini yapiga marufuku apps za wanyama.

buy fluoxetine Applications hizo zimefanya sheria za wanyama kutowekewa mkazo na kufanya ujangiri, rushwa kuongezeka kwa sababu applications hizo zinatoa taarifa kuhusu wanyama mbalimbali ambao taarifa zao zimewekwa katika applications hizo. Mamlaka husika zinataka kuweka katazo kwa applications hizo kutumika kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa watu (watalii).

get link Programu tumishi inayozungumzia masuala ya wanyama pori

Ni wazi kwamba teknolojia inapanuka siku hadi siku mpaka kufikia kutengeneza app zinazoelezea kuhusu wanyama lakini wangeni (watalii) wanatumia nafasi hiyo vibaya. Vilevile kuwepo kwa apps hizo kuna hatarisha uwepo wanyama mbugani (ujangiri kuzidi kuongezeka).

Chui1

Watalii wengi wanapenda kuendeshwa mbugani wakiona wanyama mbalimbali na kuweza kupata muonekano mzuri wa wanyama kutokana na kuzunguka mbugani huku wakipewa taarifa kuhusu wanyama wanaowaona.

Inaaminika kuwa utumiaji wa source programu tumishi hizo unaleta mkanganyiko kati ya sekta ya utalii na watalii wenyewe kutokana na kuwa yawezekana taarifa ambazo zinakuwa katika apps hizo zinaweza hazijafanyiwa masasisho (updated) ndani ya kipindi kirefu.

Kitendo cha taarifa hizo kutofanyiwa masasisho zinaweza kufanya mtalii kutojua lipi la kushika kutokana na kuwa taarifa zilizo kwenye programu tumishi ni tofauti na anayopata kutoka kwa bwana pori.

Muundaji (developer) wa applications za wanyama alitengeneza  programu tumishi ya kwanza ya wanyama akiwa na umri wa miaka 15 na hiyo ilikuwa ni kwa sababu alikuwa ni mpenzi wa kujua maisha ya wanyama mbalimbali (wild life).

Apps za wanyama zina  una faida zake kutokana na kwamba haitokuwa na ulazima wa kuzunguka mbuga nzima kuona wanyama ambao wako 5 bora (the big 5), wanaweza kupata taarifa zao kwenye apps hizo.

Kwa kupitia programu tumishi mtu anaweza kuona picha/video mbalimbali kwenye apps hizo. Je, unadhani kwa nchi kama Tanzania katazo kama hiyo inaweza kusaidia kupunguza ujangiri?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Rwanda yapiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.