Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake

Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake #Uchambuzi

0
Sambaza

Hakuna simu janja inayokuja bila kuwa na programu tumishi na zipo zile ambazo tangu kuanzishwa kwake mpaka hivi leo bado ni kinara kwa kushushwa mara nyingi zaidi. Je, unajua apps bora za muda wote? Karibu upate kuzijua leo.

go

can you buy celebrex in canada Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake..

Kuna apps nyingi sana duniani zenye watumiaji kutokana na walichovutiwa kwenye apps hizo. TeknoKona inakufahamisha kwa kina apps 5 bora za muda wote:-

 1. see url Facebook. App hii iliwekwa kwenye Google & App stores 10-7-2008 na mpaka sasa imeshapakuliwa zaidi ya watu bil. 2, app hii inapendwa na wengi kutokana na urahisi wake wa kuitumia na ni rafiki kwa wengi kwani inapatikana kwa lugha 27. Watumiaji wake wengi zaidi hadi sasa ni wa nchini Marekani (151M) ikifuatiwa na India (109M), Brazil (70M).

  Fb Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi

  Facebook

 2. Facebook Messenger. App hii ilizinduliwa Agosti 2011 na imeonekana kuwa msaada kwa watumiaji wa app hiyo kwani hakuna haja ya kuingia Facebook ili kuweza kusoma na kujibu msg kupitia Facebook kwani unaweza kama una app hii na umeunganisha na akaunti yako ya Facebook utaweza kujibu msgs zako bila kuingia FB. Hivi sasa inawatumiaji zaidi ya bil. 1.

  FB messenger

  Facebook Messenger

 3. Youtube. App hii ilizinduliwa mara ya kwanza Jan 2007 katika shughuli ya utambulisho wa iPhone uliofanywa na Steve Jobs, mwaka 2012 app hii ilianza kupatikana pia kupitia Play Store na kufanya app hiyo kupatikana kwenye Android. Kila dakika jumla ya masaa 300 ya video zinakuwa zinawekwa  (uploaded) kwenye mtandao huu, na takribani video bilioni 5 zinatazamwa kila siku. Nusu ya watumiaji wake wote wa kila siku wanatumia kupitia app yake.

  Youtube

  Youtube

 4. Instagram. App ambayo iliwafunika wengine kama Yahoo Flickr, Google Picasa ilianzishwa mwaka 2004-2005. App hii ilianza kupatikana mwaka 2010 na mwaka 2012 Instagram ilinunuliwa na Facebook. Hivi sasa app hii inawatumiaji zaidi ya bil. 1 na inapatikana katika lugha 25.

  Insta

  Instagram

 5. Skype. Skype imekuwa kimbilio la wengi kwani imewezesha watu kuwasiliana kwa nja ya video kupitia simu jaja. Hivi sasa hauhitaji kuwa na kompyuta kuweza kuipakuwa app hii kwenye kompyuta yako ili kuweza kuitumia. Marekani peke yake ina watumiaji takribani mil. 47 wa Skype.

  skype

  Skype

Ingawa ni kwa uchahe lakini TeknoKona imeweza kukufahamisha programu tumishi 5 bora za muda wote. Tupe maoni yako kuhusiana na hiki tulichokiandika.

Vyanzo: Business of Apps pamoja na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9 umefanyika
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.