Utafiti: Fahamu athari za mitandao ya Kijamii kwa watoto

1
Sambaza

Utafiti uliohusisha watoto wa umri wa miaka 10 hadi 15 wanaotumia mitandao ya kijamii kwa takribani masaa 3 kila siku umeonesha matokeo yanayoshtua.

Utafiti umeonesha watoto wanaotumia Facebook na Twitter wanajiona wanamuonekana mbaya na pia kwa kiasi kikubwa ndio rahisi zaidi kugombana/kubishana na wazazi wao zaidi.

watoto facebook

Kwa ujumla wake utafiti huu umeonesha watoto wanaotumia mitandao ya kijamii sana huwa wanajiona wabaya kimuonekano kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wale ambao hawatumii kabisa mitandao hiyo. Utafiti huu ulifanyika nchini Uingereza na ulidhaminiwa na serikali ya Uiengereza.

Utafiti ulihusisha idadi ya takribani watoto 3,500;

  • Asilimia 44 ya watoto wanaotumia mitandao hiyo kwa zaidi ya masaa 3 walisema wanagombana/bishana na mama zai zaidi ya mara 1 kwa wiki. Hii ni asilimia kubwa ukilinganisha na chini ya asilimia 22 kwa wanaotumia mitandao hiyo kidogo na wale ambao hawatumii kabisa.
  • Asilimia 53 ya watoto hao wanafurahia mionekano yao (kujiona wazuri na wasio na tatizo), hii ni asilimia ndogo ukilinganisha asilimia 82 kwa wale wanaotumia kidogo na wasiotumia kabisa mitandao hiyo.
SOMA PIA:  Microsoft Translator app yaongezwa lugha nyingine ya kutafsiri

Vipi una mtazamo gani juu ya utumiaji wa mitandao ya kijamii sana kwa watoto wa umri mdogo?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com