Axon M: Simu janja yenye vioo viwili kutoka ZTE - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Axon M: Simu janja yenye vioo viwili kutoka ZTE

1
Sambaza

Baada ya kizazi cha simu za kufunika/kufunua kupotea kwa miongo kadhaa katika soko la simu lakini hivi sasa teknolojia hiyo inaonekana inarudi kwa kasi sana baada ya Samsung kuwa na simu janja yenye vioo viwili sasa nao ZTE wanataka kuja na bidhaa kama hiyo.

Baada ya uvumi kuenea kuwa ZTE wapo kwenye mpango wa kuja na simu janja yenye vioo viwili huku ikiwa ni ya kufunua na kufunika, sasa sio uvumi tena bali ni habari ya kweli kwamba simu janja hiyo kutoka ZTE ipo njiani kuleta ushindani wa hali ya juu na simu janja zilizopo sokoni hivi sasa.

Ubora kioo ndio sifa kuu ya simu janja Axon M ambayo ina uwezo wa kuonyesha picha zenye ubora wa 1080p kwa pande zote mbili za simu hiyo.

Simu jaja Axon M kutoka ZTE.

Sifa z simu janja Axon M (Kompyuta ya kiganjani).

Katika vitu ambayo simu janja zimeshindwa kufanya na kupelekea mtu kuwa na kompyuta ni source site kutokuwa na buy colchicine tablets uwezo wa kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja (multitasking) na hivyo kuendelea kuwa changamoto kwa makampuni mengi ya simu lakini hali imekuwa tofauti kwa ZTE kwani go simu janja ya Axon M inaweza kufanya mambo mawili kwa wati mmoja.

INAYOHUSIANA  Undani wa toleo jipya la Android 9 Pie

>Prosesa. Katika hali ya kuifanya simu iwe na uwezo mkubwa wa kufanya kazi basi prosesa yake ni muhimu iwe ni ya kiwango kizuri. Prosesa iliyopo kwenye simu janja Axon M ni ileile prosesa ambayo imekuwa ikitumiwa na makampuni mengi katika miaka ya karibuni yaani Snapdragon 820.

Axon M inaweza kukunjuka kiasi cha kuwa na upana wa kioo cha kwenye tabiti (tablet).

RAM/Diski Uhifadhi. SImu janja nyingi ambazo zimekuwa ziktoka kwa muda mrefu sasa zimeonekana kuja na RAM ya juu kidogo (angalau GB 4) na ZTE hawakutaka kwenda mbali sana na kuamua kuweka RAM ya GB 4 kwenye simu janja yao inayotarajiwa kuwa gumzo. Diski uhifadhi wa kwenye Axon M ni GB 32.

INAYOHUSIANA  Motorola inatarajiwa kutoa simu janja

>Betri/Kamera. Uzuri wa simu yoyote ile ni kwamba iwe na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu na hilo linatokana na betri husika lina nguvu kiasi gani. Kwenye simu janja mpya kutoka ZTE betri lake ni nguvu kiasi cha 3,120mAh. Unaweza kukashangaa lakini simu janja Axon M ina kamera moja tu yenye 20MP.

Axon M ina uwezo wa kuonyesha programu nbili kwenye kila kioo kwa wakati mmoja.

Bei ya Axon M haijawekwa wazi lakini usitegemee kuwa itauzwa kwa bei ya kawaida kutokana na kuwa na mambo mengi ambayo simu janja zilizopo sokoni hazina. Simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 17 ya mwaka huu.

Vyanzo: The Verge, Android Authority

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|