AzamTV App yapakuliwa zaidi ya mara milioni moja

0

Programu tumishi (App) ya AzamTV ambayo ilianza kupatikana kuanzia julai mosi mwaka 2017 katika duka la Play store na Apple Store imefanikiwa kupakuliwa zaidi ya mara milioni moja kwa kipindi cha miezi sita.

Ndani ya programu tumishi ya AzamTV inamuwezesha mtumiaji kuweza kupata chaneli za Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu, ZBC 2, Azam Sports HD, Azam Sports2, Real Madrid TV na NTV Uganda kwa Tanzania pekee.

Azam TV app

Mbali na kuona chaneli hizo pia ndani ya app hiyo unaweza kusoma taarifa mbalimbali za kitaifa, kimataifa michezo, burudani na taarifa za hali ya hewa.

App ya AzamTV imeonesha mafanikio makubwa kwa muda mfupi tangu kuanza kupatikana ambapo kwa sasa kwa Tanzania inashika nafasi ya kwanza katika programu tumishi zinazopakuliwa kwa wingi na zinazozalishwa nchini Tanzania.

Na kwa zile zinazopakuliwa kwa wingi ndani ya Tanzania app ya Azam TV kiujumla inashika nafasi ya tano nyuma ya WhatsApp, Messenger, Instagram na Facebook.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com