Baadhi Ya Vipengele Vipya/Maboresho Yatakayo Kuwa Katika iOS 10! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Baadhi Ya Vipengele Vipya/Maboresho Yatakayo Kuwa Katika iOS 10!

0
Sambaza

Kama kawaida yao walivyo, kampuni ya Apple huwa hawawaangushi wateja na wadau wao kwa ujumla. iOs 10 ipo katika hatua za mwisho mwisho ili iachiwe na mpaka sasa kampuni imeshatangaza maboresho kibao

Programu endeshaji hiyo (iOS 10) itakuja na maboresho kede kede huku mambo mengine yakiwa ni mapya kabisa katika macho yetu kulingana na tulivyozoea kutumia iPhone au iPad zetu.

TeknoKona leo imekuandalia baadhi ya vipengele au mambo mapya ambayo program endeshaji mpya kutoka Apple yaani iOs 10 inatarajia kuwa navyo

http://peelingdrag.com/the-beginning-of-my-land-based-shark-fishing-journey/ 1. Meseji
Sawa unaweza ukasema mfumo wote wa kwenye eneo la meseji uko vizuri na unajitosheleza. Uko sawa kabisa lakini kampuni kama kampuni imeona hapana. Watumiaji wake inabidi wapate kilicho bora zaidi hivyo wameifanyia baadhi ya maboresho sehemu hiyo.

Baadhi ya mambo ni kama siri inaweza kutoa pendekezo la mahali pale unapoulizwa swali kama vile upo wapi sasa?. Ambapo baadala ya kuandika sehemu uliyopo unaweza ukachagua pendekezo la mahali kati ya yale siri iliyo yaonyesha. Mabadiliko mengine makubwa yamefanya katika Emoji. Mambo mengi yamefanyika hapa lakini mengi yapo katika upande ule wa iMessage.

INAYOHUSIANA  Mkebe wa kuhifadhi AirPods kuwa na uwezo wa kuchaji iPhone

http://silverspoonthaiandsushi.com/menu/italian-dishes/ 2. Loki Ya Skrini
Kampuni bado imeona kuwa mtu inabidi ufanye mambo mengi hata kama simu yako haijatolewa loki. Hapa unaweza ukaanza kujiuliza sana, kama simu haijatolewa loki kwa nini uweze fanya mambo mengi? Jibu la swali hilo sina, labda nikuambie Apple nini kitaonekana ukiwa uko eneo la skrini yenye loki

Kwanza kabisa itakuwa na muamko mpya na wa aina yake. Pia unaweza kujichanganya na ‘Notification’ za kwenye simu yako hata kwa kutumia ule mfumo wa ‘3D Touch’ lakini hii ni mpaka uwe na iPhone 6S au 6S Plus. Kwa mfano unaweza ukatumia mfumo huo wa ‘3D Touch’ kujibu meseji bila ya kufungua App yenyewe ya meseji
Pia jinsi ya kuita kamera na muziki kumebadilika. Kumbuka zamani ili kuipata kamera kiurahisi ilitubidi kuslaidi kile kialama cha muziki kidogo kwenda juu. Kwa sasa ukiwa katika eneo la control (Control canter) utaweza kuslaidi kutoka kulia kwenda kushoto ili kwenda katika muziki na kuslaidi kwenda kulia basi utaweza kufika kwenye kamera

INAYOHUSIANA  Tetesi: Muonekano wa simu mpya za iPhone

source url 3. Eneo La Picha
Kwa haraka haraka unaweza ukasema imechukua nyendo za Google. Muonekano wa eneo la picha umebadilika. Katika iOS 10 sasa App inaweza tambua vitu na mahali. Kwa mfano unaweza ukaenda katika eneo la kutafuta kisha ukatafuta vitu kama mbwa au Dar es salaam na App ikafunguka na kukuonuyesha hivyo vitu (kama vipo lakini)


‘Memories’ zimeboreshwa ambapo zinapangilia picha zako kwa kuangalia mahali upozipiga na pia la muhimu ulipiga na nani? Pia katika kila kipande cha picha zilizopigwa sehemu moja kutakuwa na kakipande kadogo kakionyesha video fupi ikiwa na tukio zima la picha mlizopiga mkiwa katika eneo ambalo mmepigia

4. Siri
Siri ni msaidizi mkubwa wa watumiaji wengi wa iPhone na iPad ambae huwa anafikiwa kwa sauti. Siri ni roboti ambayo unaweza ukaiamuru ifanye mambo Fulani Fulani na ikafanya bila matatizo. Kwa mfano unaweza ukaiambia I Google kitu chochote na ikafanya hivyo (wewe ndio boss)
Katika iOs 10 unaweza pia ukatumia Siri kutuma meseji hata kwa App zingine kama vile WeChat na WhatsApp. Licha ya hili pia kuna mengine mengi yanaweza fanywa na siri

INAYOHUSIANA  Thamani ya kampuni ya Apple imepanda


Ukiachana na haya kuna mengine mengi yamefanyika katika Apple Music, Maps na hata katika Home ambapo vifaa vya nyumbani vitaunganishwa kwa kutumia ‘Home Kit’ ambapo simu yako itakuwa na uwezo wa kuviendesha vifaa hivyo bila ya kujali ni kiwanda gani kinavitengeneza lakini cha muhimu ni kwamba vifaa hivyo vina na teknolojia ya ‘Home Kit’ tuu

a98f7300-324d-11e6-9d86-85f9eee5226c_iOS-10-home
Niambie wewe kama mwana teknolojia unategemea nini kutoka kwa iOS 10 ya Apple, niandikie hapo chini sehemu ya comment. Na pia kama kuna kipengele umekipenda katika iOS 10 pia usisite kuniandikia hapo chini. Ningependa kusikia kutoka kwako

Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari motomoto zinazohusu teknolojia kwa undani kabisa. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.