Backup and Sync: App/Programu Mpya ya Google Drive yaja

0
Sambaza

Siku chache zilizopita tuliandika kuhusu ujio wa programu mpya ya huduma ya Google Drive itakayomuwezesha mtumiaji kuweza kufanya backup ya mafaili na mafolda mengi zaidi kwenye kompyuta yake. Sasa inapatikana rasmi.

Kwa sasa haifahamiki kama Google Drive tena bali ni Backup and Sync from Google.

Programu hii mpya ni mjumuhisho wa apps/programu za zamani za Google Drive na Google Photos, app hizo hazitapatikana tena bali kazi zake zimechukuliwa na hii mpya.

google programu ya backup and sync

Muonekano wa uwezo wa kubackup maeneo mbalimbali ya kwenye kompyuta ndani ya programu ya backup and sync kutoka Google

Programu ya Google Drive kwenye kompyuta kwa kipindi kirefu iliwezesha mtumiaji kuweza kuwa na nakala ya mafaili yake salama kabisa mtandaoni kama tuu yamewekwa kwenye folda la Google Drive.

Kuanzia sasa mtumiaji ataweza kuchagua kuchagua ata mafolda mengine mengi zaidi yaliyopo kwenye kompyuta yake ata kama ni ‘Desktop’ nzima, pia kingine ni kwamba programu hii mpya itaweza kufanya backup ya hadi memori kadi na USB Drive/Flash zinazochomekwa kwenye kompyuta husika.

Unaweza kupakua programu ya Backup and Sync kutoka tovuti ya Google hapa – Backup and Sync from Google

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Samsung: Ukiwa na monitor hii uchezaji magemu utakuwa muruwa zaidi
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com