Bana Matumizi ya Intaneti kwenye Simu Yako na Hizi Mbinu..

Bana Matumizi ya Intaneti kwenye Simu Yako na Hizi Mbinu

0
Sambaza

source url Wiki zilizopita kampuni za mitandao Tanzania waliongeza gharama za kutumia intaneti. Kama unataka kuweka mambo ya bajeti safi, unaweza kutumia zana ambazo tayari zipo kwenye simu yako au kushusha programu za kusaidia kubana matumizi ya intaneti.

http://journeyfortheheart.com/?sermons-tag=sacrifice-of-praise Windows/ Lumia
Kwenye simu ya Windows 8, inaripotiwa kuwa na zana iitwayo DataSense kubana matumizi ya intaneti ila upatikanaji wa hii zana unategemea na mtandao unaoutumia. Zaidi ya hiyo, hakuna app inayojulikana zaidi kutokana na masharti ya mfumo wa windows.

image

Windows in Datasense, zana ambayo inapatikana kwenye mtandao unaoiwezesha

follow link Android
Kwenye Android kuna mbinu mbili. Mbinu ya msingi kabisa ni kutumia zana iitwayo ‘Data Usage Manager ‘ utakayoipata ukiingia ‘settings -> Data Usage’.
Kwa kutumia Data Usage Manager unaweza:
– Kuchunguza matumizi yako kwa ujumla.
– Kutambua app gani zinatumia data zaidi ili uchukue hatua zaidi.
-Kuzuia intaneti kwa app usizotumia. (Hii inarefusha chaji pia).
– Kujiwekea notisi pale intaneti (bando) linapoelekea kuisha.
– Kuipangilia simu Kukata kabisa intaneti pale bando linapoelekea kuisha.

image

Zana ya Data Usage ya Android itakusaidia sana kubana matumizi ya Intaneti

Njia ya hii ya kubana matumizi inahitaji kuifanya mara kwa mara na inafaa kama tabia yako ya kuwezesha intaneti inafanana kila siku. Kama ungependa chaguzo zaidi tumia app ya My Data Manager na Onavo Data Count ambazo teknokona inaziamini.

INAYOHUSIANA  Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

iOS
Kwa simu na ipad za Apple, njia ya msingi ni kuingia kwenye Settings > Cellular. Ingawa hautaweza kuweka kiwango cha mwisho au kupata notisi juu ya matumizi kama ilivyo kwenye Androidi, utaweza kuamua app ipi iweze kutumia intaneti kati ya zile ulizozipakia.
Unaweza kuzuia app kutumia intaneti kimya kimya kwa kuingia kwenye Settings->General > Background App Refresh.
Pia, unaweza ukaingia kwenye  settings->Notifications na kupunguza matumizi ya intaneti kupitia notisi za app zako.

image

Kwa msaada zaidi, wasiliana nasi kupitia teknokonatz (at) gmail dot com au kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply