BarraCuda Pro: Diski uhifadhi ya ukubwa wa TB 12 kwa ajili ya kompyuta za mezani

0
Sambaza

Mwaka hadi mwaka makampuni mbalimbali yamekuwa yakijitahidi kutengeneza vifaa vya kuhifadhi vitu mbalimbali kwenye simu/kompyuta zetu au kwenye kifaa kingine chochote cha kiteknolojia.

Seagate ni moja ya makampuni yanayofahamika sana kwa utengenezaji wa vifaa vya kuhifadhi vitu kadha wa kadha vyenye ukubwa tofauti ambapo mara nyingi vifaa hivyo hutumika kwenye kompyuta za mezani au kompyuta mpakato, yaani Laptop.

Seagate imelenga HDD ya TB 12 itumike kuhifadhi vitu vya ubora gani?

DIski uhifadhi ya Terabyte (TB) 12 ni wazi kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kuchukua data nyingi sana na mpaka mtu awe amefanikiwa kuifanya diski uhifadhi ya TB 12 kujaa basi vitu vilivyomo humo ndani ni vingi sana.

SOMA PIA:  Jinsi Ya Kurekodi Uso Wa Skrini Ya iPhone (iOS 11*) Ikiwa Imeambatana Na Sauti! #Apple

Kwa wanajihusisha na masuala ya uhariri wa picha za mnato au picha za kiwango cha hali ya juu basi diski uhifadhi ya TB 12 kutoka Seagate ndio itakuwa chaguo sahihi kuweka kwenye kompyuta yako.

Diski uhifadhi ya TB 12 kutoka Seagate mahususi kwa kompyuta za mezani.

BarraCuda Pro ina uwezo wa kuhifadhi video za ubora wa 4K, picha zilipigwa kwenye kamera ya Canon toleo jipya (DSLR) ambapo lenzi yake ina 120MP, video za kiwango cha nyuzi 360, video zinazotokana na teknolojia ya Augmented Reality (AR), Virtual Reality (VR).

Diski uhifadhi mpya kutoka Seagate ina kasi ya 7200RPM pamoja na kuwa na 256MB cache memory jambo ambalo litafanya kompyuta yako kuwa na kasi sana pale unapokuwa ukihamishia mafaili kwenye kompyuta.

Seagate wanaonekana kuja na diski uhifadhi ya TB 12 ni muendelezo wa kuenedlea kuleta diski uhifadhi za kiwango cha juu zaidi huku ikiwa na mipango ya kuwa na diski uhifadhi wa ZB 163 (Zettabytes 163) kufikia mwaka 2025.

SOMA PIA:  Mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga

DIski uhifadhi ya BarraCuda Pro inapatikana kwa $530|Tsh. 1,191,970 na dhamana ya miaka mitano mara baada ya kununua. Je, wewe ni mmojawapo kati ya wale ambao watanunua diski uhifadhi BarraCuda Pro kutoka Seagate?

Vyanzo: The Verge, ExtremeTech, PetaPixel

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com