Basi linalopita juu ya magari lafanyiwa majaribio China.

0
Sambaza

Basi linalopita juu ya magari mengine limefanyiwa majaribio huko China wiki hii kwa mujibu wa BBC, basi hilo ambalo linaweza kupita hata katika foleni kubwa za magari kwa kupita juu yake linaweza kubeba hadi abiria 300.

ad_214620212-e1470224023880

Uzinduzi wa basi hilo

Miezi kadhaa iliyopita wazo la basi linalopita juu ya magari ambalo  linatembea huku likiruhusu magari kupita uvunguni kwake lilioneshwa katika maeonesho ya Teknolojia beijing, wazo hilo sasa limefanyiwa kazi na hatimaye basi hilo limefanyiwa majaribio wiki hii katika mji wa Hebei.

SOMA PIA:  Kampuni yashtakiwa kutokana na Headphones zinazofanya ujasusi kwa watumiaji wake

Mambo machache unayopaswa kuyafahamu juu ya basi hili!

  1. Basi hili linatembea katika reli maalumu ambayo inaweza kutandawza katika barabara ambazo tayari zimekwisha anza kutumika.
  2. Gharama ya kufanya basi hili lianze kazi ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za kuanzisha usafiri wa kasi wa treni ama mabasi ya mwendokasi. Hii inaufanya mfumo huu wa usafiri kuwa na nafasi kubwa kuja kutawala sekta ya usafirishaji mijini.
  3. Basi hili linaweza kwenda hadi kilomita 60 kwa saa na mabasi haya yanaweza kuungwa na kufikia manne kwenda pamoja.
  4. Basi hili moja linaweza kufanya kazi ya mabasi hadi manne ya mwendokasi makubwa.
  5. Bado haijajurikana ni wapi hasa mabasi haya yatatumika nchini china lakini tayari mihemko kwa wananchi ambao wameonekana kufurahishwa na mfumo huu mpya wa usafiri.
  6. Basi hili litatumia nishati ya umeme badala ya nishati ya mafuta.
SOMA PIA:  VW yajipanga kuhamia katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme

Tazama vidieo fupi kuelezea basi hilo linalopita juu ya magari hilo hapa chini


Ingawa ni bado mapema kujua kama aina hii ya usafiri wa mjini unaweza kusambaa na kufika katika nchi zetu za Afrika mashariki lakini ni wazi kwamba hii inaweza kuwa suluhusho kwa matatizo ya usafiri hasa katika miji yetu.

Endelea kufuatilia teknokona kwa habari mbali mbali za teknolojia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com