BBM300: Gari hili spesheli linafyatua matofali 300 kwa dakika! #Teknolojia

0
Sambaza

Mara nyingi wagunduzi na watengenezaji wa vitu huja na mawazo mazuri sana pale wanaposhindana dhidi ya chambamoto iliyo mbele yao. Na wazo zima la kutengeneza gari hili spesheli, BBM300, lenye uwezo wa kufyatua matofali 300 kwa dakika ndivyo lilivyokuja kwa mfanyabiashara mmoja huko nchini India.

Bwana Satish mwaka 2007 alichoka kuona hali ya kuwalipa wafanyakazi wengi kwa kazi ya kufyatua matofali na kisha wafanyakazi hao kuwa wavivu sana na kutoonekana kazini mara kwa mara.

bbm300

Gurudumu la kati ndio lenye jukumu la kupanga matofali chini kwenye ardhi.

Akaanza kutafuta njia nyingine ya kuongeza uzalishaji bila kuathirika na tatizo la wafanyakazi, na hapo ndio akaanza kuwekeza katika utengenezaji wa gari lenye uwezo wa kufyatua matofali.

Ufanyaji kazi

 

gari la kutengeneza matofali bbm300

Gari hilo likifanya kazi, vipuli vingi vilivyotumika katika utengenezaji huu uligharimu pesa nyingi na ilimbidi avinunue, hivyo alijikuta akiwekeza pesa zake nyingi sana mwanzoni.

Gari linasehemu kubwa ya kuhifadhi mchanganyiko wa mchanga na simenti ambao kisha utusukumwa na kwenda kwenye gurudumu spesheli ambalo linazunguka na kupanga tofali moja moja gari likiwa linatembea.

Toleo la kwanza walilipa jina la BBM150 ambapo gari lilikuwa na uwezo wa kutengeneza matofali 150 kwa dakika na hivyo kutengeneza hadi matofali 40,000 kwa siku.

SOMA PIA:  Google yakiri kuwafuatilia watumiaji wa simu janja za Android

Toleo jipya ni BBM300 ambapo lina uwezo wa kutengeneza matofali 300 kwa dakika, na hivyo kuweza kutengeneza hadi matofali 85,000 kwa siku.

Angalia video ikionesha utendaji kazi wake

Mashine hii imejizoelea umaarufu nchini India na tayari amechukua hakimiliki ya teknolojia hiyo na ameweza kupata oda za kuuza hadi nchini Nepal. Tayari imejipatia umaarufu unaovutia kupata msaada wa uwekezaji na labda ndani ya miaka michache mashine hizi zitasambaa zaidi.

Vipi je una mtazamo gani juu ya teknolojia hii?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com