StoreDotFlashBattery: Betri inayojaa chaji chini ya dakika moja! #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

StoreDotFlashBattery: Betri inayojaa chaji chini ya dakika moja! #Teknolojia

0
Sambaza

Katika jambo linawalowakera wanaomiliki simu janja ni simu zao kuishiwa na chaji mapema jambo linalowalazimu kutembea na chaji ya ziada kama power bank au kuwa na simu ya ziada inayotunza chaji kwa muda mrefu. Yote hayo chimbuko lake ni betri ya simu husika.

watch

SImu ikiwa inakaa na chaji kwa muda mrefu ni jambo la kufurahisha na hata kupelekea mtu kuipenda simu yake mara dufu. Katika teknolojia ya betri za simu hivi sasa kuna betri lenye uwezo wa kujaa chaji chini ya dakika moja 😯 😯 . Teknolojia hiyo iliwekwa kwenye maonyesho mara ya kwanza mwaka 2015 na kampuni ya Israeli ya StoreDot.

Teknolojia iliyotumika

Betri hiyo imetengenezwa kwa teknolojia mpya kabisa inayowezesha kuchaji simu kwa haraka sana kwa kufanya chaji kusafiri kutoka upande wa Anode kwenda upande wa Cathode.

StoreDotFlashBattery, betri inayochaji simu janja chini ya dakika moja.

Mwaka 2015, kampuni iliyotengeneza betri hiyo iliweka picha jongefu mtandaoni ikionyesha betri hiyo ikichaji simu janja aina ya Samsung chini ya dakika moja na aliyetengeneza betri za StoreDot flash pamoja na chaji yake ni mfanyakazi wa zamani wa SanDisk ambaye pia alishiriki katika utengenezaji wa diski uhifadhi kutoka SanDisk.

Upatikanaji wake

http://downtowntowing.com/?p=815 Teknolojia hiyo tayari inafanyiwa majaribio na watengenezaji betri wawili China na kwamba utengenezaji kwa wingi wa betri hizo unatarajiwa kuanza robo ya kwanza ya 2018 ingawa lengo la kampuni hiyo kutoka Israeli ni kwenda mbali zaidi na kuweza kuchaji betri za magari yanayotumia umeme ndani ya dakika tatu! Hata hivyo StoreDot walizindua betri ya gari ambayo inajaa chaji kwa dakika tano katika maonyesho ya teknolojia mjini Berlin.

INAYOHUSIANA  Ujio wa HTC U12 Life haupo mbali sana

watch Soma pia: Betri lenye uwezo wa kuzima moto!

Mafanikio hayo mpaka sasa yalitokana na kukushanya $48.5m kutoka kwa wadau mbalimbali wa teknolojia, $10m kutoka kwa kampuni inayomilikwa na tajiri Roman Abramovich (mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu, Chelsea).

Hakuna kitu kisichokosolewa kwani tayari kampuni imebezwa kwa kuambiwa kuwa mpango wa huo hautofanikiwa kutokana na kwamba hiyo si mara ya kwanza, makampuni mbalimbali yalishajaribu na wakashindwa ila StoreDot wana imani kuwa mpango wao utafanikiwa.

Vyanzo: BBC, Psfk

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.