Ujenzi wa betri kubwa kuliko yote mpaka sasa wakamilika kwa 50%

2
Sambaza

Ni bilionea ambaye anajishughulisha na vitu mbalimbali, Bw. Elon Musk na sasa ameamua kuishangaza duniani kwa kuamua kujenga betri kubwa kuliko zote duniani ambalo litatumika kuzalisha umeme na wananchi hawatalipia hata shilingi kupata huduma hiyo 🙄 🙄 .

Kwa miaka kadhaa sasa Bw. Elon Musk ameamua kujikita zaidi katika utengenezaji wa vitu mbalimbali ambavyo vitaweza kusaidia watu wa hali ya chini. Na sasa yupo katika mpango wa kukamilisha kutengeneza betri kubwa kuliko yote kwa kushirikiana na Neoen (muundaji wa nishati inayoweza kutumika tena na tena wa Ufaransa) pamoja na serikali ya Australia.

Mahali ambapo miundombinu ya betri hiyo itajengwa. Betri hilo linatarajiwa kukamilika ndani ya siku 100 na litakuwa na nguvu ya kufanya nyumba takribani 30 elfu kuwa na umeme huko Kusini mwa Australia.

Ushirikiano wa Musk na Neoen katika ujenzi wa betri kubwa zaidi duniani.

Katika makubaliano ya Bw. Musk na Neoen ni kwamba Tesla itajenga betri hiyo (mpaka sasa limeshakamilika kwa 50%) na kwa upande wa Neoen, mitambo yake inayotumia nishati ya upepo itatumia betri hiyo kuzalisha umeme. Betri hilo la aina ya  Lithium-ion lina nguvu kiasi cha megawatt 100.

Katika mpango huo pia utahusisha uwekejaji wa jenereta za dharura ambazo zitatumika kuongeza ufanisi wa vyanzo vingine vya umeme kama vile kinu cha kuzalisha umeme kinachotumia nishati ya umeme wa Jua, umeme wa gesi.

tesla betri

Tesla wameshinda zoezi hili kupitia tenda. Kwa kiasi kikubwa kampuni hiyo imewekeza sana katika teknolojia za betri kutokana na uhitaji wa mabetri mazuri kwenye magari yao yanayotumia umeme

Kampuni ya Tesla ambayo ilitumia moja ya betri zake zinazotumika kwenye magari yake kuwasha umeme  kwenye kumbi ya muda ya starehe ambapo Bw. Musk alitangaza mpango huo.

Betri hilo likikamilika litakuwa limewasaidia wananchi kutolipa kiasi cha jumla ya $50 milioni kwa mwaka kuhakikisha wanapata nishati ya umeme kutokana na kwamba huduma hiyo itakuwa ikipatikana bure huko Kusini mwa Australia.

Vyanzo: The news in color, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Udanganyifu unaoweza kusababisa 'ukaibiwa kidigitali' wabainika kwenye bidhaa za Apple
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com