Betri zinazotumiwa katika simu zinatoa sumu kibao! #Utafiti - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Betri zinazotumiwa katika simu zinatoa sumu kibao! #Utafiti

0
Sambaza

Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha vifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu na laptop, utafiti wagundua.

betri za simu laptop betri la simu

http://soudavar.org/category/air-jordan/air-jordan-3 Mabetri ya teknolojia ya Lithium-ion ni maarufu zaidi

Utafiti huo uliofanyika nchini China ulibaini get link gesi 100 zenye sumu kali zinatolewa na betri za aina ya Lithium-ion. Baadhi ya gesi hizo ni pamoja na kaboni monoksaidi (CO), ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.

Watu wengi wanaotumia vifaa vya elektroniki vinavyotumia betri za teknolojia ya lithium-ion hawafahamu madhara ya kutotumia betri zenye ubora na pia betri kupata joto kupita kiasi (overheating), hasa hasa pale vinapochajiwa. Haya yamesemwa na watafiti hao kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Czech pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China.

Soma Pia – Ukiona haya, Fahamu muda wa Kubadilisha Betri la simu yako umefika!

order flagyl cheap Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri iliyo chini ya asilimia 50 ya chaji.

betri zinatoa sumu

Utafiti huu unaonesha kuna umuhimu wa kuondoa simu yako kwenye chaji mara tu inapojaa, na pia si vizuri kulala na simu iliyojaa karibu yako. Tutaendelea kufuatilia kuona kama watafiti wengine watakubaliana na matokeo haya

Katika utafiti huo mpya, walichunguza aina ya betri za Lithium-ion. Mabetri haya ndiyo yamekuwa yakisifiwa sana kiusalama na yanatumika kwenye vifaa vingi zaidi vya elektroniki. Utafiti huu unaweza fungua milango ya uchunguzi zaidi unaoweza sababisha maboresho ya teknolojia nzima ya utengenezaji wake.

Soma pia;

Tuambie mtazamo wako juu ya utafiti huu.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Vyanzo: BBC, Battery University

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.