Bibi wa miaka 81 atengeneza app yake ya kwanza kwa ajili ya iOS - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Bibi wa miaka 81 atengeneza app yake ya kwanza kwa ajili ya iOS

0
Sambaza

Kuna mtu anakwambia umri wa mtu ni kigezo cha mtu huyo kujifunza mambo ya kidigitali? Mwambia hayupo sahihi, bibi kizee wa miaka 81 azindua app kwa ajili ya watumiaji wa iOS/iPhone.

 Bibi wa miaka 81
Bibi huyu mwenye jina la http://stupidbeat.com/new-music-mac-miller-prince-sole-childish-gambino/ Masako Wakamiya wa nchini Japani alianza kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza takribani miaka 21 iliyopita, akiwa na umri wa miaka 60. Kuhusu suala la kazi ingawa sasa hivi ni mstaafu ila ameshawahi kufanya kazi benki kwa muda wa miaka 43.
buy discount Finax App yake yenye jina la Hinadan, ametengenezwa kwa ajili ya wajapani kama sehemu ya kuizimisha utamaduni wa nchini humo ujulikanao kama Hinamatsuri (yaani Girls’ Day – Siku ya wadada). App hiyo ingawa ni kama gemu lengo kuu lake ni kuwafundisha watu jinsi ya kupangilia midoli yao mbalimbali sahihi kwenye maonesho ambayo huwa yanafanyika katika maadhimisho ya utamaduni wa Girls’ Day.
Mtu anakuwa anashinda katika gemu hilo kama akifanikiwa kuipanga midoli hiyo kwa usahihi kabisa.

Muonekano wa maonesho ya madoli katika maadhimisho ya Girls Day

Muonekano wa gemu hilo

Bibi huyo hajafanikiwa katika hili tuu kwenye eneo la masuala ya kidigitali, bali anamiliki pia blogu ambazo anaandika kwa lugha ya kijapani na kiingereza ambapo huwa anazungumzia masuala ya ubunifu kwa kutumia programu ya Excel na pia huwa anazungumzia safari mbalimbali za matembezi ambazo huwa anafanya.
see Unaweza pakua app yako kutoka soko la App Store – iTunes/iOS

Uzee mwisho wapi tena? Una mtazamo gani juu ya mafanikio ya huyu bibi? Tuambie maoni yako na usisahau kushare..

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.