Bill Gates: Niliwazuia watoto wangu kutumia simu mpaka wafikishe miaka 14

0
Sambaza

Muanzilishi wa kampuni ya Microsoft na tajiri namba moja duniani William henry maarufu kama Bill Gates amefichua kwamba aliwazuia watoto wake kutumia Simu mpaka walipofikisha umri wa miaka 14.

Bill Gates ana watoto watatu aliozaa na Mkewe aitwae Melinda Gates. Bill na Melinda walifunga ndoa yao mwaka 1994.

Soma pia – Mambo 16 Ya Ukweli Wa Kuvutia Kuhusu Bill Gates!

airtel tanzania bando

Watoto wa Bill Gates ni Jennifer Katharine mwenye umri wa miaka 20, Rory John mwenye umri wa maika 18 na Phoebe Adele mwenye umri wa miaka 14. Rory ndio mtoto pekee wa kiume wa Bill Gates.

Miaka michache iliyopita Bill Gates akiwa na familia yake

Bill Gates anasema watoto wake walikuwa alipowazuia kutumia simu kabla ya kufikisha miaka 14, wakilalamika kudai kutaka kutumia simu kama watoto wengine walioanza kutumia simu wakiwa na umri mdogo.

SOMA PIA:  Zima "Automatic updates" kwenye simu yako

Bill Gates kama mzazi mwingine anasema aliweka kanuni kwa watoto wake kutowanunulia simu mpaka watakapofikisha umri wa miaka 14.

Anaongeza kusema Bill Gates wakati alipokuwa akihojiwa na The Mirror kwamba mara zote walipanga muda mzuri kwa watoto kuangalia Televisheni au Kompyuta, ambapo iliwasaidia kupata muda muafaka wa kulala.

Hata marehemu Steve Jobs wa Apple aliwahi kueleza kuwazuia watoto wake kutumia Simu wakiwa na umri mdogo.

Suala la umri gani ni sahihi kwa mtoto kuanza kupewa simu bado limekuwa na mkanganyiko kwa familia nyingi. Wengine wanasema kuanzia miaka 8 mpaka 12. Wengine kuanzia miaka 13 mpaka 18. Bado hakuna umri sasa uliokubaliwa kwa pamoja. je wewe unafikiri ni umri gani ni sahihi wa kuanza kutumia simu?

SOMA PIA:  Matumizi ya mitandao ya kijamii huchochea upweke! #Utafiti

Soma pia – Mambo 16 Ya Ukweli Wa Kuvutia Kuhusu Bill Gates!

Je unakumbuka ulikuwa na umri gani wakati unanunua simu yako ya kwanza ya mkononi? Ushawahi kumnunulia simu mtoto wako au mjukuu wako akiwa na umri gani? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com