BitCoin yazidi kung’ara; thamani yake yazidi kuongezeka

0
Sambaza

Mfumo wa kufanya malipo kwa kutumia BitCoin ambao unatumika sana katika nchi zilizo katika dunia ya kwanza na ya pili lakini hata kwa nchi zilizopo kwenye dunia ya tatu ingawa si kwa kiasi kikubwa kulinganisha na nchi zilizo nje ya bara la Afrika.

Katika ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa thamani ya BitCoin 1 imefikia karibu dola za kimarekani 4,890 (zaidi ya Tsh. 10,750m). Kwa tafsiri isyo rasmi BitCoin ni pesa ya kidigitali inayotumika kufanya malipo ya aina yoyote bila kulipa ada ya tozo.

BitCoin iliundwa na Satoshi Nakamoto mwaka 2008 na kuanza kutumiwa na wengine mwaka 2009. Satoshi Nakamoto ambaye ni mtumiaji wa intaneti lakini kwa siri sana hivyo kufanya mpaka leo kumjua mtu huyo ni nani hasa kiundani. Kujua mengineyo kuhusu BitCoin INGIA HAPA.

BitCoin imetokea kupendwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na urahisi wa kufanya malipo ya aina mbalinbali bila ya kutozwa ada.

Thamani ya BitCoin mpaka sasa imetabiriwa kuwa itaendelea kuongezeka na hivyo kuendelea kuleta ushindani dhidi ya dola ya kimarekani na pesa nyinginezo. Hata hivyo, wapo walitabiri kuwa thamani ya BitCoin itakuja kushuka na kufikia kiasi cha chini ya $3,000 (zaidi ya Tsh. 6.6m). Kwa ujumla wa pesa zote za kidigitali thamani yake imefikia $170bn.

SOMA PIA:  Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

Kwa takwimu za mwezi  Julai kulikuwa na BItCoins 16.5m kwenye mzunguko wa kifedha ikiweka rekodi na kufikia $1,268 (mwezi Machi) kwa mara ya kwanza. Kwa matazamio ya mbali thamani ya BitCoin itakuwa juu zaidi miaka mitano ijayo.

Chanzo: Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com