Blackberry Kutoa Toleo La Simu Itakayotumia Android!? - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Blackberry Kutoa Toleo La Simu Itakayotumia Android!?

0
Sambaza

Inasemekana kampuni ya BlackBerry inafikiria kuanza kutengeneza simu ambazo zitatumia Android kama mfumo wa uendeshaji (OS) kwa mara ya kwanza. Imesemekana kwa muda mrefu ata baada ya kuja na toleo la BlackBerry OS 10 hii ikiwa ni pamoja na kuleta simu mpya kadhaa bado hawajaweza kutengeneza faida katika eneo la biashara ya simu. Wameshindwa kuwarudisha wapenzi wa bidhaa za kampuni hiyo ambao walichotwa na bidhaa za Apple na simu janja nyingine zinazotumia Android.

blackberry-z30-front

Simu ya blackberry Z30

Watu wa ndani ya kampuni hii wameliambia shirika la habari la reuters kwamba kampuni hiyo inafanya uamuzi huo ikiwa ni mkakati wa kuupa tafu mfumo wake wa usimamiaji wa apps na mawasiliano. Mfumo huu wa usimamizi wa programu na vifaa uliopewa jina la BES12 ni mfumo ambao unategemewa kutumiwa na Taasisi za serikari na mashirika ya umma kwaajiri ya kusimamia vifaa sio tu vya blackberry bali hata vya Apple na Android. Mfumo wa BES unahakikisha usalama wa data za mtumiaji wa simu husika katika mawasiliano.products-bes12-control-center.png.original

INAYOHUSIANA  Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor

Iwapo Blackberry watatoa kweli toleo la simu inayotumia mfumo wa uendeshaji wa Android basi  watakuwa wamepeleka ujumbe tosha kwa wale wote ambao walikuwa wanamashaka na mfumo huo (unaokuja)  wa usimamizi wa programu na vifaa (BES12) kwa kusema kuwa itakuwa vigumu kwa blackberry kusimamia vifaa vinavyotengenezwa na mifumo ya uendeshaji tofauti na ule wao wanaotumia yaani wa blackberry.

Tangazo la mfumo wa usimamizi wa programu na vifaa wa BES12

Pengine blackberry watatumia mfumo wa uendeshaji wa Android katika simu yao mpya inayotegemea kutoka hivi karibuni, simu hiyo mpya ni simu ya ku-slide na pia itakuwa na skriini ya kugusa(touch screen) huku ikiwa na baadhi ya vitufe vya mfumo wa QWERTY. Hata hivyo blackberry haijasema mengi juu ya simu hii mpya ambayo ilitangazwa mwezi machi mwaka huu.

INAYOHUSIANA  TTCL na vifurushi vya usiku

eb70d288-e5cb-44a7-bbd3-14a7b76d38b6-620x372

Kwa sasa BlackBerry imekuwa ikishindwa katika vita yake ya kibiashara dhidi ya makampuni simu za Android na Apple. Imelazimika kupunguza nguvu kazi yake kutoka wafanyakazi 17,500 mwaka 2011 hadi wafanyakazi 6,225 kwa mwaka huu. Blackberry imekwisha toa matoleo mengi ya simu kama Blackberry z30, z10, Bold series na Curve Series.

here Ulikuwa mtumiaji wa BlackBerry na ukahama? kama ndiyo tuambie je habari hii itakurudisha kumiliki BlackBerry yenye Android?, na kama wewe hujawai kutumia BlackBerry je upo tayari kujaribu toleo hilo jipya? Usisite kutuandikia maoni yako.

[socialpoll id=”2276589″]

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply