BlackBerry yafikiria Kuachana na biashara ya Simu – bado hawatengenezi faida

0
Sambaza

Kwa miaka miwili sasa kampuni ijulikanayo kama Blackberry imekuwa ikipata hasara katika uuzaji wa simu janja kutoka kampuni hiyo.

Kwa zaidi ya miaka miwili Blackberry imekuwa ikipata hasara. Blackberry ni kampuni maarufu sana kwa utengenezaji wa simu janja, ni kampuni kutoka Canada na imeripotiwa kuwa Blackberry wamepata hasara ya dola milioni 670 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

John Chen-Mkurugenzi Mtendaji wa Blackberry blackberry yafikiria

John Chen-Mkurugenzi Mtendaji wa Blackberry

Hata hivyo katika matoleo ya simu janja za Blackberry zilizotoka hivi karibuni waliamua kutumia programu endeshaji ya Android bado simu zao hazifanyi vizuri katika mauzo, simu za BlackBerry kwa sasa zinashikilia chini ya asilimia 1 ya soko la dunia.

Moja ya simu janja zinazotengenezwa na Blackberry zenye kutumia Android

Moja ya simu janja zinazotengenezwa na Blackberry zenye kutumia Android

Asilimia kubwa ya mapato wanayopata yanatokana na utengenezaji wa programu endeshaji ambazo zinatumika katika mambo ya kiusalama na hivyo kama kampuni wanafikiria kuachana na biashara ya utengenezaji wa simu janja na kuzidi kuwekeza zaidi kwenye biashara inawaingizia faida zaidi badala ya kuedelea kupata hasara.

SOMA PIA:  Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017

Je, wewe ni mpenzi wa simu janja kutoka Blackberry? Tuambie nini maoni yako kuhusiana na uamuzi ambao Blackberry wanataka kuuchukua? Endelea kufuatilia kutoka hapahapa Teknokona nasi tutazidi kukuhabarisha.

Chanzo: Telegraph, BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com