Bluetooth 5.0 – Kasi ya mara 2 zaidi, umbali wa mara 4 na ukubwa wa mafaili wa 800% zaidi

0
Sambaza

Teknolojia ya Bluetooth ni moja ya teknolojia iliyokwenye vifaa vingi zaidi vinavyotumika. Hii ni kuanzia kwenye simu, kompyuta na laptop..

Na sasa kupitia Bluetooth 5.0 teknolojia hiyo imefanyiwa maboresho makubwa na kuifanya bora zaidi kuliko ilivyo sasa.

bluetooth 5.0

Maboresho ya teknolojia hayo yataanza kupatikana katika vifaa vingi vitakavyokuja kuanzia mwishoni mwa mwaka huu, 2016 na mapema mwaka 2017.

Maboresho yanayokuja katika Bluetooth 5.0

  • Kasi ya utumaji wa mafaili utaongezeka mara dufu – mara mbili
  • Umbali wa kuweza kuunganisha vifaa viwili umeongezwa mara nne zaidi.. zaidi ya mita 360!
  • Na inaonakana muda si mrefu utaweza kutuma pia mafaili makubwa zaidi (asilimia 800 zaidi ukilinganisha na hali ya sasa)
SOMA PIA:  Gari linaloweza kupaa kama ndege, suluhisho la muda kwa mahali unapoenda

Je wajua teknolojia ya Bluetooth inaendeshwa na kina nani?

Matengenezo na maboresho ya teknolojia nzima ya Bluetooth inasimamiwa na shirika linalofahamika kwa jina la Bluetooth Special Interest Group (SIG). Hili ni kundi la makampuni mbalimbali yenye kunufaika na teknolojia hiyo, kwa sasa inahusisha watu na makampuni 30,000…hii ni pamoja na Apple, Intel, IBM na Microsoft. Suala lote la utumiaji wa teknolojia hiyo pamoja na kutoa leseni kwa yeyote anayeitaji kuitumia linasimamiwa na SIG. Makao makuu yao yapo Kirkland, Washington, Marekani.

SOMA PIA:  Saa ya kisasa isiyochajia na kitu chochote bali na joto la mwili wa binadamu

 

Teknolojia ya Bluetooth imekuwa muhimu sana kwa sasa, hii ni kuanzia kwenye simu, kompyuta, spika janja, saa janja na vifaa vingine mbalimbali.

Vyanzo: IBTimes na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com