Brazil: WhatsApp Ilipofungiwa Kwa Muda, Telegram Ilipata Zaidi ya Watumiaji Milioni 1.5 Wapya

1
Sambaza

Je unaweza kukaa masaa 48, yaani siku mbili bila kutumia huduma ya WhatsApp kwenye simu yako? Ni vigumu.

Nchini Brazil huduma ya WhatsApp ilijikuta ikifungiwa kwa masaa 48 na Serikali ya nchi hiyo kutokana na kukataa kutoa data za watumiaji wake kwa serikali ya nchi hiyo.

Kifungo hicho hakikufanikiwa kuduma sana kwani baada ya takribani masaa 12 walifanikiwa kushinda kesi kwenye mahakama ya rufaa na hivyo huduma hiyo kurudi hewani kama kawaida.telegram-vs-whatsapp

Huduma nyingi za mitandao zimekuwa zikijikuta katika kutofautiana na Serikali nyingi duniani katika suala la wao kuvipa ruhusu vyombo vya usalama kuchungulia data (namba za simu, mazungumzo n.k) za watumiaji wao.

SOMA PIA:  Emoji mpya 2017 zinakujia, zifahamu mpya zinazokuja

Nchini Brazil inasemekana WhatsApp inatumika katika zaidi ya asilimia 92.5 ya simu zote nchini humo, na kabla ya tukio hili mpinzani wake, app ya Telegram – ilikuwa imepakuliwa kwa takribani asilimia 2.5 tuu. Lakini baada ya tukio la WhatsApp kutopatikana app ya Telegram ilipakuliwa kwa zaidi ya mara milioni 1 ndani ya masaa machache nchini humo.

“WhatsApp inakadiria kuwa na jumla ya watumiaji milioni 100 nchini Brazil”

Jaji wa mahakama ya rufaa katika hukuma yake ya kuilazimisha serikali kisheria kurudisha huduma za WhatsApp nchini humo alisema ‘kwa kuheshima misingi ya katiba ya nchi hiyo haileti maana kuwanyima huduma muhimu mamilioni ya watu kwa sababu tu ya kampuni husika kukataa kutoa data zilizoombwa na Serikali’.

SOMA PIA:  Siri: Programu ya Apple yaita ambyulensi kumsaidia mtoto

Mark Zuckerberg, wa Facebook – inayomiliki WhatsApp, alisema kwa kipindi kirefu Brazil imekuwa mfano mzuri wa taifa linalopigania ukuaji wa teknolojia na huduma ya intaneti, na hatua ya jaji mmoja kuwapa adhabu watumiaji mamilioni wa huduma hiyo kisa tuu WhatsApp imeamua kulinda data za watumiaji wake ni uamuzi wa ajabu.

Nchini Brazil kuna matumizi mengi ya WhatsApp ukitoa utumiaji wa watu wa kawaida, huduma ya WhatsApp inatumiwa pia na vyombo na mashirika ya Serikali na mengineyo katika kuwasiliana na wanaowatumikia/hudumia. Wabunge wengi wa nchi hiyo walipinga vikali uamuzi huo wa kuifungia.

SOMA PIA:  AzamTV App yapakuliwa zaidi ya mara milioni moja

Telegram ndiyo iliyonufaika zaidi na uamuzi huu. Telegram ni huduma nyingine ya mawasiliana kama vile WhatsApp ila ikiwa na tofauti kadhaa. Ndani ya masaa machache Telegram walidai wamepata zaidi ya watumiaji milioni 1.5 kutoka nchini Brazil, baadae walisema wamepata jumla ya watumiaji milioni 5 wapya. Inaaminika wengi wao ni kutoka nchini Brazil.

Telegram inawatumiaji zaidi ya milioni 60 duniani kote, namba hii ndogo ukilinganisha na WhatsApp yenye watumiaji zaidi ya bilioni 1….ingawa wengi wanakubali Telegram ina sifa na uwezo mzuri zaidi ukilinganisha na WhatsApp.

Soma Pia – Je App Gani ni Zaidi Kati ya WhatsApp na Telegram ktk Kuchati?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Brazil yaifungia WhatsApp tena! - TeknoKona

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com