Tovuti ya video za ngono wadukuliwa na taarifa za watumiaji kuwekwa wazi

Tovuti ya video za ngono wadukuliwa na taarifa za watumiaji kuwekwa wazi

0
Sambaza

Watumiaji wa moja ya tovuti/mtandao mkubwa wa video za ngono duniani, Brazzers.com wiki hii watakuwa katika hali ngumu kisaikolojia baada ya data za kuwahusu kuwekwa wazi na wadukuzi.

Data hizo zinawahusu takribani watumiaji 800,000 wa tovuti hiyo na data zinajumuhisha majina ya watumiaji hao na taarifa zao zingine kuhusu wapendavyo ndani ya tovuti kubwa hiyo ya ngono.

video za ngono

follow site Utazamaji wa picha na video za ngono unafanywa kwa siri na watu wengi sana, inategemewa jambo hili litawafedhehesha sana watumiaji wa tovuti hiyo

http://builtriteconstruction.com/?p=5 Inasemekana udukuzi wa data hizo ulifanyika mwaka 2013 ila ni sasa ndio wadukuzi hao wamehamua kuweka wazi data za watumiaji wa tovuti hiyo. 

go

Udukuzi wa kuingilia mifumo yote ya data ulifanyika baada ya kufanikiwa kudukua eneo la mazungumzo (forums) la tovuti hiyo. Wadukuzi waliweza kuingilia njia hiyo kutokana na wasimamiaji wa tovuti ya Brazzers kutosasisha mfumo mzima unaotumika kutolea huduma za forums – unafahamika kwa jina la vBulletin.

Katika swali ambalo TeknoKona imeuliza watembeleaji wake kwa zaidi ya miezi 15 inaonekana ata Tanzania utumiaji bado upo juu. Zaidi ya asilimia 70 kati ya watu zaidi ya 200 walioshiriki kujibu walisema washawahi au bado wanatembelea mitandao ya ngono.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

[socialpoll id=”2256886″]

Tovuti hiyo ilikuwa inatumia tolea la vBulletin la nyuma na hivyo kuwa na makosa flani ya kiusalama ambayo wadukuzi waliyatumia kuweza kuiba data za watumiaji wa tovuti nzima.

Teknokona inakushauri uwe unabadilisha mara kwa mara nywila (passwords) za tovuti unazotumia, pia kumbuka kutumia huduma za mtandao kwa mambo yanayojenga zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.