BrighterMonday Yaleta Mapinduzi Katika Soko La Ajira Tanzania!

0
Sambaza

Labda nikuulize, huwa unatafuta vipi ajira? Je unatumia mtandao au huwa unaenda katika ofisi husika?

Kama unatumia mitandao mbali mbali ni vizuri zaidi kwani una uwezo mkubwa sana wa kuona nafasi mbalimbali zikitangazwa. Kingine kikubwa cha kukumbuka ni kwamba dunia inabadilika na kuwa katika hali ya udigitali zaidi.

Miaka michache tuu ijayo kuanzia sasa kompyuta na vifaa vingine vya kielektroniki vitafanya karibia kila kitu kwa ajili yetu.

BrighterMonday

Baada ya kusema hayo je unawajua BrighterMonday? Huu ni moja kati ya mitandao mikubwa sana na yenye nguvu isiyo ya kifani katika swala zima la kutafuta ajira Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

BrighterMonday inalenga zaidi kusaidia wale wanaotafuta kazi kwa kurahisisha kutafuta na kuomba kazi husika. Kingine kikubwa ni kwamba BrighterMonday bado itakuwa mstari wa mbele katika kuoanisha sifa za watafutaji wa kazi punde tuu ajira mpya zitakapotangazwa.

SOMA PIA:  Matangazo kwenye simu: Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye simu za Android

Shusha App Ya BrighterMonday Jobs katika soko la Google Play Store Bureeee kabisa!
Sifa Za App Hii Ni Pamoja Na
• Utapata kutafuta ajira bila kuingia kwenye akaunti yako
• Kutafuta na kuomba kazi ukiwa popote pale
• Kutengeneza wasifu wako (CV)
• Utajulishwa punde tu ajira mpya zinazoendana na vigezo vyako zikitangazwa

Ripoti zinasema zaidi wa asilimia 10 ya watu milioni 55 Tanzania hawana ajira. Pengine hili linabaki kuwa ni tatizo kwani watu wengi hawajui kama kuna App maalumu kama vile ile ya BrighterMonday  ambayo inaweza kumsaidia mtu kupata kazi kwa urahisi kabisa.

Kingine cha kuangalia ni kwamba kuna nafasi chache sana za ajira kuliko idadi ya watu ambao wanatafuta ajira, hili linapelekea BrighterMonday kuwapa jukwaa waajiri waweze kutangaza nafasi za ajira na kisha wanaotafuta ajira waweze kuingia katika jukwaa hili na kuchagua nafasi kulingana na sifa zao.

SOMA PIA:  Twitter: Ina watumiaji wazungumzaji sana lakini Haitengenezi Pesa

“BrighterMonday imekuwa chanzo cha bure cha ajira na fursa za kazi kwa wanaotafuta kazi nchini Tanzania tangu ilipozinduliwa mwaka 2009. Tumekuwa tukiboresha teknolojia zetu ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi wanaotafuta kazi Tanzania. Tuna tovuti nzuri sana ambayo inatumika kirahisi hata kwa kutumia simu za mkononi. Hivi sasa, zaidi ya 62% ya watumiaji wetu wanatupata kwa kutumia simu za mkononi. ” – Alisema Meneja masoko wa BrighterMonday, Lugendo Khalfan.

Brighter Monday

Tanzania ni moja ya nchi ambayo ina muamko mkubwa sana katika swala zima la teknolojia hasa kwa matumizi ya vifaa vya kiganjani hivyo kitendo cha BrighterMonday kuanzisha App ni cha aina yake kwani kinakuwa ndio mkombozi wa wengi kwa nyakati hizi.

SOMA PIA:  Kuusoma ujumbe uliofutwa na aliyeutuma kwenye WhatsApp inawezekana!

App ya BrighterMonday Jobs ni dhahiri itongeza ubunifu wa kampuni katika kuendana na ukuaji wa teknolojia kwenye biashara.

Pakua App mpya ya BrighterMonday Jobs leo na ujipatie ajira yako!

Tumia App hii alafu tuambie umeipokeaje? Hii ni moja ya App za muhimu kabisa kuwa nazo katika kifaa chako, ningependa kusikia kutoka kwako. Niandikie Hapo chini sehemu ya comment

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus
Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com