App zinazuhusisha michezo ya kuuliza maswali ya kusisimua lakini yanayohusisha ukweli almaarufu kama ‘Trivia’ ni mizuri. Lakini kwa muda mwingine yanakuwa na maswali ya ajabu ajabu ambayo mara nyingine yanabeba taarifa zisizo na maana kwa mfano unaweza ulizwa swali kama ‘waandishi wa teknokona huwa wanakula chakula gani?”.
Ndio, unaweza ulizwa swali kama hilo, lakini nafikiri hakuna mtu anaejali hayo. Kama unataka kujibu maswali magumu zaidi na yenye changamoto za kutiisha basi huna budi kuijaribu App ya Brilliant. App ambayo inakupa maelfu ya maswali katika ulimwengu wa sayansi, hesebu na mantiki yote hayo kwa ajili yako. Licha ya kupewa taarifa ambazo hazina maana kutoka katika michezo mbalimbali ya Trivia, utakuwa unaiweka akili yako katika hali (afya) nzuri na hata uwezo wa kufikiria utaongezeka.
Ngoja Nikupe Mfano Ujionee Aina Ya Maswali Yanayoulizwa
Baada ya kudhani unalijua jibu bofya “Check answer.” ili kuangalia kama umepatia au umekosea na pia unaweza bofya “view solution” ili kuona njia.
Unavyozidi kujibu maswali ndivyo unavozidi kupanda chati/ngazi. Pia uunaweza kujiunganisha na wenzio ambao wanatumia App hii ya Brilliant na kuanza kushindana
MUHIMU: Ukijiunga kutumia app ya Brilliant, utapokea barua pepe nyingi sana na mara nyingine inakuwa hadi zaidi ya moja kwa siku. Lakini hili sio tatizo kwani utakuwa na uwezo wa kujiondoa katika orodha ya wale wanaozipata barua pepe hizo (za kukera) kwa kujiondoa yaani ‘ unsubscribe’
Brilliant – iOs – Shusha
Brilliant – Android – Shusha
Nina imani kuwa tukipunguza kucheza magemu mengine katika simu ambayo hayana maana na kuanza kutumia App kama hii (Brilliant) katika kuweka vichwa vyetu sawa itatusaidia sana.
One Comment