CarbFix: Wanasayansi wageuza hewa ya sumu kuwa jiwe. #Sayansi

0
Sambaza

Watafiti wanaoendesha uchunguzi katika eneo la Iceland, wanaamini kuwa wanaweza kupunguza hewa chafu inayochafua mazingira kwa kunasa hewa ya sumu ya Carbon Dioxide (CO2) na kuigeuza kuwa mawe.

Wanasayansi hao waliyeyusha hewa hiyo ndani ya maji kupuliza mchanganyiko wake ardhini, ambako ilichanganyika na madini ya Volcano na kuunda mawe yanayofanana na chokaa.

carbfix

CarbFix: ‘Formula’ ya kisayansi inayowezesha teknolojia hiyo kufanikiwa

Wanasayansi hao wamesema mfumo huo unaweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya viwango vya joto duniani kwa sababu mawe ya Volcano inayohitajika kugeuza gesi hiyo yanapatikana kote duniani.

SOMA PIA:  Tegemea Mambo Haya Katika Toleo La iOS 11! #MaelezoNaPicha

Utafiti huo wa kugeuza hewa chafu kuwa jiwe ambao umechukua muda wa miaka miwili uligharimu takriban dola milioni 10. Wanapendekeza kuwa hiyo itakuwa njia thabiti ya kupambana na tabia nchi japo itagharimu pesa nyingi.

Wanasayansi wageuza hewa ya sumu kuwa jiwe

CarbFix: Wanasayansi wageuza hewa ya sumu kuwa jiwe

Mradi huo unaotambuliwa kama “CarbFix” unaweza kunasa hewa ya sumu kutoka angani na kuipenyeza kupitia kwenye mabomba na maji hadi ardhini. Shughuli hiyo inakamilika kwa asilimia 95% ya hewa hiyo kuganda na kuwa jiwe.

SOMA PIA:  Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake!

Ni wazi kuwa utafiti huu utasaidia sana maeneo ambayo yapo karibu na viwanda hivyo kufanya watu kuepuka kuvuta harufu mbaya kutoka viwandani na kuwafanya watu kuugua magonjwa mbalimbali kutokana na kuvuta hewa zenye kemikali na kiwango kikubwa cha CO2.

Teknolojia hiyo… endelea kutembelea TeknoKona na tutaendelea kukuletea habari kuhusu maendeleo ya teknolojia hii.

Vyanzo: https://www.or.is/english/carbfix-project na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com