CES 2016: LG Kuonesha Kioo (screen) Chao cha Kukunja - TeknoKona Teknolojia Tanzania

CES 2016: LG Kuonesha Kioo (screen) Chao cha Kukunja

0
Sambaza

LG wanaonesha katika maonesho ya CES 2016 (Consumer Electronics Show) screen ya nchi 18 ambayo unaweza kuikunja na kama vile unavyokunja gazeti, hii ni baada ya kufanikiwa kutenganisha sakiti na kioo.

follow

http://maricaevents.com/tag/venue/ LG sio kampuni ya kwanza kuonesha teknolojia hii ya screen ya kukunja lakini ni wazi kwamba wao wanakuja na kitu tofauti na yale ambayo makampuni mengine yamekuwa yakionesha siku za huko nyuma.

CES LG

see Screen ya LG inayokunjika kama gazeti

Ingawa LG walidokeza juu ya teknolojia hii katika maonesho kama haya mwaka jana lakini mwaka huu wataonesha taarifa zaidi juu ya teknolojia hii kitu ambacho kinaonesha wako tayari zaidi kuleta teknolojia hii mpya katika bidhaa.

INAYOHUSIANA  Apple kununua vioo vya simu kutoka LG badala ya Samsung

Pamoja na hii LG pia wataonesha TV yao nyembamba zaidi ya inchi 55 na pia TV yenye uwezo wa kuonesha picha katika pande mbili (nyuma na mbele) ambayo itafaa sana kwaajiri ya mabango ya maduka nyakati zijazo. Screen hizi zote zinatumia teknolojia ya OLED (soma makala hiyo hapa) ambayo tuliiongelea katika moja ya makala zetu kipindi kilichopita.

Bado haijajulikana ukubwa na resolution ya screeni hii mpya ya kukunja ila mara ya mwisho kampuni hii ya kiKorea ilionesha screen yenye ukubwa wa sm3 na yenye resolution za pixel 1200×810. Matarajio ya wengi ni kwamba LG watakuja na ukubwa na resolution kubwa zaidi ya hii.

CES+2016_18+inch+Rollable+OLED

Screen ya inchi 18 inayoweza kukunjwa

Hii teknolojia ya screen ya kukunja itapata matumizi mengi pindi itakapokuwa imekamilika, vifaa kama laptop ambavyo vinachukua nafasi kubwa tukivibeba vitabadilika na kuanza kutengenezwa kuturuhusu kuvikunja ili tusiwe na mizigo mikubwa. Utakumbuka kwamba kampuni hii ndiyo walio kutengeneza keyboard ya kukunja (soma makalahiyo hapa)ambayo ilikuwa maalumu kwaajiri ya simu janja, hii itakuonesha kwamba safari ya kutengeneza vifaa vyepesi kubebeka inazidi kupatakasi na huenda tukaanza kuona kompyuta za kukunja mapema kuliko tulivyodhania.

INAYOHUSIANA  Apple kununua vioo vya simu kutoka LG badala ya Samsung

CES (Consumer Electronics Show) 

Haya ni maonyesho makubwa ya teknolojia zinazotumiwa na wateja zaidi hasa za electronics, maonesho haya hufanyika nchini Marekani kila mwaka na mwaka huu yanafanyika jijini Vegas. Maonyesho haya hutumiwa na makampuni mbalimbali kwaajiri ya kutangaza bidhaa zao mpya, pia hutumiwa na wabunifu wadogo wadogo. Teknokona itakuletea habari kuu kutoka katika maonesho haya makubwa hivyo kaa mkao wa kupata habari.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply