Chanjo ya Zika kujaribiwa kwa binadamu kwa mara ya kwanza

0
Sambaza

Kampuni moja ya  madawa imepata kibali cha kufanya majaribio ya chanjo ya Virusi vya Zika kwa binadamu, majaribio haya ni ya kwanza na yanalenga kuona jinsi ambavyo dawa hii inapokelewa na miili ya binadamu.

zika-virus-vaccine

Kama majaribio haya yatafanikiwa basi yatakuwa mafanikio makubwa katika kuelekea kuzuia kabisa gonjwa hili ambalo ni tishio kwa dunia. Mpaka sasa ugonjwa huu umesambaa zaidi katika nchi za Amerika ya kusini na pia Amerika ya kati.

SOMA PIA:  Sidiria kwa ajili ya kugundua saratani ya matiti. #Afya

Jarida la PHILADELPHIA  limeripoti kwamba chanjo hii itajaribiwa kwa wafanyakazi arobaini ambao hawana maambukizi ya ugonjwa huo ili kuangalia jinsi miili itakavyo jibu baada ya kupewa chanjo hiyo. Huu ni utaratibu wa kawaida kabla ya chanjo kutumika kwa wagonjwa hujaribiwa ili kuona kama inamazara gani kwa binadamu wa kawaida.

Matokeo ya majaribo haya ya watu arobaini yatatangazwa baadae mwaka huu na matokeo haya yatatoa mwelekeo wa kufanikiwa ama kushindwa kwa chanjo hiyo.

brazil-zika-virus

Mtoto mwenye shida ya microcephaly ambayo inahusishwa na virusi vya zika.

Chanjo hii inatengenezwa na kampuni ya Inovio Pharmaceuticals Inc ambayo inashirikiana na GeneOne Life Sciences Inc, mnamo mwezi wa Februari shirika la afya duniani lilitangaza ugonjwa huu kuwa ni janga la dunia.

SOMA PIA:  Taasisi ya Sayansi China yakuza mpunga mpya wenye urefu wa mita 2.2

Virusi vya Zika vinaaminika kuwa na uhusiano na watoto kuzaliwa na matatizo kama microcephaly ambayo husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo.

Je unauelewa ugonjwa wa virusi vya Zika? tujuze unachokifahamu kuhusu ugonjwa huu na pia utuambie umejisikiaje baada ya wanasayansi kupiga hatua katika kupata chanjo.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com