Chanzo cha Tatizo la Intaneti kwa Baadhi ya Makampuni Leo!

1
Sambaza

Baadhi ya mitandao ya simu kama vile Vodacom imeathirika katika eneo la huduma ya intaneti kwa siku ya leo. Baada ya uchunguzi wetu kwa kuwasiliana na baadhi ya vyanzo vyetu vya habari tumepata kufahamu tatizo ni nini hasa.

Inasemekana tatizo lipo kwa upande wa mtoaji mkubwa wa huduma ya intaneti SEACOM. Seacom ni mtandao mkubwa wa waya kubwa za huduma ya intaneti (Fiber) anayeunganisha huduma hiyo ya intaneti kwa Tanzania na mataifa mengine. Inasemekana mitambo yao imekuwa na hitirafu na inashungulikiwa.

SEACOM ni moja ya chanzo kikubwa cha huduma ya intaneti kwa biashara kubwa kama vile mitandao ya simu na makampuni mengine yanayotoa huduma hiyo.

SEACOM ni moja ya chanzo kikubwa cha huduma ya intaneti kwa biashara kubwa kama vile mitandao ya simu na makampuni mengine yanayotoa huduma hiyo.

Hivyo kama wewe ni mteja wa Vodacom au mtandao mwingine wa simu/huduma na umekuwa unapata shida ya kutumia huduma hiyo basi fahamu hii ndio sababu ya tatizo ilo, na inategemewa mambo yatawekwa sawa.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

1 Comment

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com