Cheza Mpira Wa Kikapu Katika App Ya Facebook Messenger! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Cheza Mpira Wa Kikapu Katika App Ya Facebook Messenger!

0
Sambaza

App ya Facebook Messenger imekua na maboresho kadha wa kadha tangia ilipozinduliwa mwaka 2011. Kutoka katika kutuma na kupokea meseji na sauti za kawaida tuu mpaka kuwa na vipengele kadhaa

enter site

watch Hii inamaanisha kuwa kwa sasa Facebook Messenger haihusishi kutuma na kupokea ujumbe, sauti na picha tuu kwa mfano sasa watu wanaweza wakapata huduma ya kupiga simu ndani ya Messenger hiyo.

follow site Kwa sasa mtandao huo maarufu zaidi, Facebook kupitia App yake ya Messenger  imeamua kuonggeza kipengele katika App hiyo.  Kuna gemu la siri ambalo linaweza likachezwa na marafiki.

Gemu La Mpira Wa Kikapu

Gemu La Mpira Wa Kikapu

Gemu hili linachezwa hivi: Mchezaji ataweza kecheza mchezo huu kwa kutupia mpira katika nyavu, kila atakaposhinda atapata chansi ya kwenda mbele zaidi. Kwa mfano atakapo ingiza mipira 10 kwenye nyavu ataweza kwenda katika sehemu nyingine (Level).  Ili kufanya gemu kuwa gumu kadri mtu anavyoendelea kucheza, Goli litakuwa linatokea katika maeneo mbali mbali katika skrini.

INAYOHUSIANA  Punguza kupokea maombi ya urafiki Facebook

Wachezaji pia wanaweza wakashindana ndani ya App hiyo ili kujua nani ameshinda sana katika kutupia mipira golini.

Hii sio mara ya kwanza kwa Facebook Messenger kuanzisha kamchezo Fulani kwa watumiaji wake. Hata mwaka jana walianzisha gemu ya Chess, ambayo inawezwa kuchezwa kwa kuandika @FBChess katika uwanja wa maongezi.

FBChess

FBChess

Kama unataka kupata michezo hii cha kwanza kabisa hakikisha unalo toleo jipya kabisa la Facebook Messenger.

Mitandao ya kijamii inakua sana siku hizi na mipya mingi inaanzishwa ili mtu kujihakikishia kuwa namba moja inabidi ubuni ufanyike. Ubunifu ambao utamfanya mtumiaji wa mtandao huo kuweza kubaki katika mtandao huo. Kwa mfano ukiingia katika mtandao wa TeknoKona una uhakika wa kupata habari mbalimbali za kiteknolojia kila siku (habari moto moto) sasa kwanini usibaki?

INAYOHUSIANA  Facebook katika ulimwengu wa mahaba

Tuambie sehemu ya comment je ulishawahi kucheza gemu hii au ndio kwanza unaisikia? Naamini kuna vingi katika mitandao hii ya kijamii kuliko kuchati tuu. Tembelea TeknoKona Kila Siku kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.