China kujenga Kituo Kikubwa cha Utafiti chini ya Bahari - TeknoKona Teknolojia Tanzania

China kujenga Kituo Kikubwa cha Utafiti chini ya Bahari

0
Sambaza

China wametangaza mpango wao wa kujenga kituo kikubwa kabisa cha utafiti chini ya bahari ya Kusini mwa China, kitakachosaidia katika masuala ya tafiti mbalimbali.

Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa katika umabli wa futi 9,800 (au kilometa 3) chini ya maji na kinatajwa kuwa kitashika namba 2 katika orodha ya mipango (projects) 100 mikubwa inayohusu masuala ya sayansi na teknolojia.

Changamoto ni muda gani wataalamu watatumia kukamilisha ujenzi wa kituo hicho lakini pia gharama zitakazotumika katika project hiyo ukizingatia ni moja ya projects kubwa kuwahi kufanywa na China.

Changamoto nyingine ni uwepo wa wanyama wakali chini ya bahari na sehemu ambayo kituo hicho kinategemewa kujengwa.

Moja ya meli kubwa ya kijeshi inayomilikiwa na China

cheap avodart uk Moja ya meli kubwa ya kijeshi inayomilikiwa na China

source site Ujenzi wa space station hiyo utadumu kwa miaka mitano na imeelezwa kuwa kituo hicho kitakuwa kikitumia kufanya tafiti za kisayansi kama vile kutafuta madini na mafuta yanayopatiana katika bahari ya Kusini mwa China.

INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

Iwapo project hiyo ikikamilika itasaidia sana katika kuliimarisha taifa la China katika jeshi, sayansi lakini pia na teknolojia na hivyo kujihimarisha na kuzidi kuwa moja ya mataifa yenye nguvu duniani. http://myownclarity.com/2015/10/ Kwa mfano kuna wanaoona uamuzi huu kuwa wa kibabe kwani eneo la bahari ya kusini mwa China mipaka yake inagombewa na mataifa mengi, hii ikiwa ni China, Ufilipino, Malaysia, Japani na Vietnam.

utafiti chini ya bahari

China na Utafiti chini ya Bahari: Eneo hilo la bahari linalopangwa kutumiwa na China lina ugomvi mkubwa wa mipaka baina ya mataifa mengi ya eneo hilo

Kwa hakika ujenzi wa kituo hichi utaweka historia kubwa katika uweze wa kiujenzi, sayansi na kiutafiti..kwani jambo kama hili bado halijawahi fanyika. Tutazidi kukuhabarisha kuhusiana na ujenzi huu.

INAYOHUSIANA  Uhai wa tafiti za kisayansi nchini Uingereza

Je, China watafanikiwa kujenga kituo hicho? Endelea kufuatilia Teknokona nasi tutazidi kukuhabarisha kuhusu hili na mengine mengi.

Chanzo: Bloomberg, Popular Mechanics(PM) na NatureWorldNews

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.