China yawasha mtambo wa umeme wa nguvu za jua unaoelea ziwani

0
Sambaza

China imewasha mtambo wa umeme wa nguvu za jua ambao unaelea ziwani, mtambo huo ambao umekwisha kamilika ni kielelezo tosha cha nia na madhumuni ya China kuwa taifa kubwa katika nishati mbadala.

umeme wa nguvu za jua unaoelea ziwani

Umeme wa nguvu za jua unaoelea ziwani

Kwa mujibu wa jarida la Mashable mtambo huu ambao unaelea katika ziwa ambalo lilitokana shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe, unajumuisha paneli 160000 ambazo kwa pamoja zinatengeneza Mega watt 40 utakuwa ndio mtambo wa umeme wa nguvu za jua ambao unaelea.

SOMA PIA:  Axon M: Simu janja yenye vioo viwili kutoka ZTE

Kabla ya kukamilka mtambo huu Uingereza ndiyo ilikuwa inamiliki mtambo mkubwa wa umeme wa nguvu za jua unaoelea ambao ulikuwa unatoa Mega watt 6.3.

airtel tanzania bando

Mtambo wa kufua umeme kwa nguvu ya jua ikiwa imefungwa katika maji inakuwa na faida kadhaa, kwanza maji husaidia kupooza paneli jambo ambalo husaidia kuongeza ufanisi wa mitambo, pia kufunga mitamo katika ziwa ama bahari huokoa ardhi kavu yenye matumizi mengi kutumika kwaajiri ya kuvuna umeme na mwisho paneli zinapofungwa katika ziwa hupunguza kiasi cha maji kinachogeuzwa kuwa mvuke baada ya kuwakiwa na jua.

SOMA PIA:  Mfumo wa AI utakaoweza kufanya kazi bila intaneti unaundwa

China imekuwa ikitumia kiwango kikubwa zaidi cha pesa katika kujaribu kuwekeza katika nishati mbadala baada ya kuwa inaongoza katika kiwango cha uzalishaji hewa ukaa. Nchi hiyo ndiyo inatajwa kuwa ndio taifa linaloongoza katika nishati mbadala hasa baada ya Marekani kujitoa katika ushirika wa Paris,  tayari China imejiwekea lengo la kuhakikisha kwamba 11% ya nishati zake ni nishati mbadala.

Endelea kufuatilia mtandao wa Teknokona upate taarifa mbalimbali za teknolojia kama zinavyotokea ulimwenguni.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com