China wafanya majaribio ya ndege ya kwanza ya abiria kutengenezwa nchini humo

0
Sambaza

Biashara ya utengenezaji ndege za abiria nchini China inaonekana kuanza kuchukua sura mpya baada ya mafanikio ya kufanya majaribio ya ndege ya kwanza kabisa kwa ajili ya abiria. Hii italeta ushindani kwa makampuni makubwa kama vile Boeing na Airbus – ya Marekani na Ulaya.

China yatengeneza ndege ya abiria ya kwanza: Hii ndiyo C919

China yatengeneza ndege ya abiria ya kwanza: Hii ndiyo C919

Wiki iliyopita kwa mara kwanza kabisa China walifanikiwa kufanya majaribio ya ndege hii kubwa inayolenga kuwa mwanzo wa utengenezaji wa ndege za abiria nchini humo.

SOMA PIA:  Matumizi ya simu janja pamoja na 'Drones' katika kupambana na Malaria

Kwa kiasi kikubwa mafanikio haya kwa China yatasaidia kushusha gharama kubwa ya ununuaji wa ndege za usafiri mpya kutoka barani Ulaya na nchini Marekani.

Tayari ukuaji wa teknolojia ya utengenezaji magari na mabasi kwa nchini China umesaidia kwa kiasi kikubwa watumiaji wa mataifa mengi duniani kote kuweza kupata eneo mbadala la kununua vyombo hivyo vya usafiri kwa bei nafuu – ukilinganisha na bei kutoka makampuni ya Ulaya.

Ndege hii inatengenezwa na kampuni iendayo kwa jina la Comac na safari ya majaribio hewani ilichukua muda wa lisaa limoja na ndege hiyo ilirudi salama bila tatizo lolote.

SOMA PIA:  FAHAMU: Mega Pixel (MP) Ni Nini Na Inafanya Nini Katika Picha!

Je ni salama?

China yatengeneza ndege: Katika majaribio yake ya kwanza hewani yalichukua muda wa lisaa limoja; tayari kampuni ya Comac ina oda mbalimbali za aina hii ya ndege

Kama inavyofahamika vipuri vingi vya ndege ni muhimu viwe vya ubora kweli kweli kwani kosa dogo tuu linaweza sababisha ajali mbaya sana.

Sehemu muhimu za ndege kama vile injini, sehemu kuu ya marubani, na eneo la chini la ndege (belly) vyote vimenunuliwa kutoka makampuni nguli kwenye vipuri vya ndege ya nchini Marekani na Ulaya – kama kampuni ya General Electric na Honeywell.

Ndege hiyo inayotumia ‘code’ ya C919 ina uwezo wa kubeba abiria 158 na utengenezaji wa teknolojia nzima hadi kufikia kuikamilisha ndege hii imechukua miaka kumi.

SOMA PIA:  Kaspersky yakiri kupakua nyaraka za siri za Marekani

Hadi sasa hivi tayari kampuni hiyo imepata oda za ndege 570 za jamii ya C919 kutoka kwa wanunuaji 23. Wengi wao wakiwa ni makampuni ya ndege ya nchini China na mengine nje ya nchi.

china yatengeneza ndege ya abiria

Tayari kazi inaendelea ya kutengeneza ndege ya pili na inategemewa kasi itazidi kuongezeka kwa kila utengenezaji unavyoendelea

Ndege hii kushindana na familia ya ndege za Airbus 320 na Boeing 737.

Je wewe una mtazamo gani juu ya maendeleo haya yanayofikiwa huko nchini China.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com