Chromebase for Meetings kutoka Google pamoja na Acer

0
Sambaza

Google wakishirikiana na Acer wameleta kifaa kipya kwaajiri ya video conferencing, kifaa hiki ni kompyuta ambayo imetengenezwa mahususi kwaajiri ya kuendesha mikutano baina ya watu ambao wapo maeneo tofauti.

chromebase

Kifaa hicho ambacho kina skrini ya inch 24  ambayo ina resolution ya 1080 ambayo ni touch screen na pia kifaa hiki kitakuja na vinasa sauti ama microphone nne kwaajiri ya kukamata sauti kwa wakati mmoja.

Chromebase itaweza kuendesha mkutano ambao una hadi  pande 25 kwa wakati mmoja huku pande hizo 25 zikiwa sehemu mbali mbali kwa kutumia app ya hangouts.

SOMA PIA:  Ifanye kompyuta yako ukiiwasha ikuite jina lako. #Maujanja #Windows

Chromebase inakuja kwa gharama ya dola 800 za kimarekani ambapo hii ni pamoja na warantii na gharama za msaada wa kiufundi kwa mwaka mzima. Uzuri wa kifaa hiki ni kwamba kinaweza kutumika kama Chromebook ya kawaida.

chromebase

Muonekano wa Chromebase kwa nyuma.

Google wametoa Chromebase ili kuwapa chaguo wateja wake ambao walikuwa wanatamani kuwa na Chromebox lakini wakashindwa kutokana na bei ya chromebox kuwa juu saana. Chromebox ambayo nayo ni kwaajiri ya video conferencing lakini yeneyewe vifaa kama kamera vinakuja tofauti havijaungwa pamoja, Chromebase litabaki kuwa ndiyo suluhisho la pekee ambalo ni la bei nzuri.

SOMA PIA:  Makampuni 10 Yanayoongoza Kupata Maombi Ya Kazi Kupitia LinkedIn! #Teknolojia

Chromebase ni mahususi kwa maofisi ambayo yana ofisi zao ndogo mikoani ama nchi jirani kwani ni rahisi kuonganisha na kufanya mkutano kwa ofisi zote ilimradi tu kuna intaneti nzuri.

Lakini pamoja na yote Google wameleta pia huduma ya kuweza kutunza vifaa vya mikutano vya Chrome, huduma hii itarahisisha swala zima la wamiliki wa hivi vifaa kutunza na kuelewa vifaa vyao vina hali gani hata kama vipo mbali saana.

Vyanzo: Mbalimbali pamoja na Engadget

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com