Clips - App mpya kwa ajili ya iPhone na iPad - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Clips – App mpya kwa ajili ya iPhone na iPad

0
Sambaza

Apple ambao wanasifika kwa kutoa vitu vya bei ghali na hata apps zao kupakuliwa kwake mpaka ulizipie hivi karibuni wamezindua programu tumishi iitwayo Clips mahususi kwa ajili ya kutengeneza video na picha kwa ajili ya kutumika kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Instagram.

http://wordsplusmusic.com/?p=1

follow url clips

go to link Clips ambayo inategemewa kuleta ushindani katika soko la apps kutokana na mazuri na urahisi wa kutumia app hiyo ukizingatia wamelenga zitumike kwenye zile apps pendwa nikimaanisha Facebook na Instagram.

Sifa za Clips

Clips pia inampa mtumiaji urahisi wa kuunganisha picha, video fupi(clips), muziki na kufanya kuwa video na kuweza kuwashirikisha wengine kupitia app ya ujumbe mfupi wa maneno kutoka Apple au kushare kwenye Istagram, Snapchat au hata Facebook.

Programu tumishi ya Clips inamuwezesha mtumiaji kuweza kutengeneza picha jongefu (video) za ‘urefu wa kujidai’…yaani ambazo sio fupi.

Kwenye app ya Clips kuna kipengele cha Live Titles kitakachowezesha kueleza video hiyo inahusu nini; itakuwa na kicha cha habari.

Live titles inamuwezesha mtumiaji kutengeneza kichwa cha habari kwa kutumia sauti yake na pia kufanya muonekano wa vidoe kuwa kama katuni.

Clips itaanza kupatikana kwenye App store mwezi Aprili na itapatikana bila malipo. Inafanya kazi vyema kwenye iPhone 5s na matoleo mengineyo pamoja na matoleo mbalimbali ya iPad.

Vyanzo: Telegraph, pamoja na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.