Coca Cola waweka zaidi ya bilioni 2 kutafuta sukari bora zaidi! #Shindano

0
Sambaza

Kampuni kubwa ya soda duniani, Coca Cola, wameweka dola milioni 1 za Kimarekani (zaidi ya Tsh bilioni 2) kwa ajili ya shindano la kuja na sukari mbadala ya kutumika kwenye soda zake.

Kwa miaka mingi changamoto kubwa kwenye biashara ya soda imekuwa ni aina ya sukari inayotumika kwenye bidhaa hizo. Imepewa lawama kubwa kuwa chanzo cha magonjwa hatari kama vile matatizo ya kisukari na mengineyo.

Kampuni ya Coca Cola imeweka shindano ambalo mtu yeyote anaweza kushiriki – kazi kuu ni kuja na sukari ambayo inaweza kutumika kwenye vinywaji vyake ambayo ni salama, pia ambayo haitokani na kemikali za viwandani – inatakiwa iwe imetokana na vyanzo ‘natural’.

SOMA PIA:  Sidiria kwa ajili ya kugundua saratani ya matiti. #Afya

Coca Cola waweka zaidi ya bilioni 2 kutafuta sukari bora zaidi! Kwa nini Coca Cola wameweka shindano hili?

Inasemekana wanywaji soda wamezidi kupunguza utumiaji wao wa vinywaji vya soda kutokana na sababu za kiafya. Kwa Marekani pekee wastani wa unywaji wa soda vya kila mtu mmoja umeshuka kutoka takribani lita 140 kwa mwaka hadi kwenye lita 100 kwa mwaka.

coca cola pepsi

Wastani wa idadi ya mauzo ya lita za soda kwa mwaka kwenye makampuni yote (Coca Cola na Pepsi) yanaporomoka nchini Marekani

soda

Wastani wa utumiaji wa soda (lita) kwa mtu mmoja kwa mwaka unaendelea kuporomoka

Coca Cola na ata makampuni mengine kama vile Pepsi tayari wameelewa ili kujihakikisha ukuaji wa soko lao kwa miaka ya baadae ni lazima watatue suala la aina ya sukari inayotumika kwenye vinywaji vyake. Watumiaji wengi siku wanakunywa kwa kuelewa hatari za kiafya zinazoweza patikana kutokana na unywaji mwingi wa soda.

SOMA PIA:  Njia mpya ya kujikinga na maambukizi ya VVU kwa wasichana kufanyiwa majaribio Afrika

Je wewe una mtazamo gani juu ya shindano hili? Je kwa wastani unatumia vinywaji vya soda mara ngapi kwa wiki?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com