Ifahamu app ya Cosmic Watch. App yenye uwezo wa kueleza mengi kuhusu mfumo mzima wa Jua ambao unajumuisha Jua, sayari, nyota, mwezi.
Kwenye app hii utapata maelezo ya kina kuhusu ni lini mfumo mzima wa Jua uliundwa kutokana na sayansi inavyoeleza. Pia kuweza kupata masasisho kuhusu yaliyogundulika hivi karibuni kwenye mfumo mzima wa Jua kwa ujumla wake.
App hii ni muhimu kwa yoyote anayependa kujua zaidi kuhusu Jua, sayari, nyota na vinginevyo vilivypo angani lakini pia ni muhimu sana kwa wanafunzi wanajifunza jiografia kutoka ngazi ya chini mpaka vyuoni kutokana na kwamba ndani ya app hii itamsaidia kujua mengi zaidi kuhusu mfumo wa jua na kujiongezea wigo mpana wa kuelewa.
App hii inauzwa katika masoko ya apps, na bei ni kwenye Tsh 7,500/= hadi Tsh 10,000 na inapatikana kwa Android na iOS.
Pakua (Download – App hii inauzwa)
Google PlayStore | AppStore (iOS)
Tutaendelea kukujuza iwapo maboresho yatafanyika katika app hii ili na wewe msomaji wetu uweze kujua kuhusu maboresho hayo kutoka katika tovuti yako pendwa: teknokona.com.
Vyanzo: live science, tech times